Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ni mkombozi Afrika Mashariki


 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka JICA. Ujumbe huo umetembelea wagonjwa pamoja na miradi mbalimbali  ya kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo leo.
 Wageni kutoka JICA wakiwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru. Kutoka kushoto ni Ofisa wa Hospitali Kuu ya Shonan Kamakura, Emiko Shiono,  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JICA Idara ya Afrika, Komori Masakatsu, Mwakilishi wa Afrika nchini Japan, Milanga Mwanatambwe na Meneja wa Tiba, Injinia Katsumasa Shirai.
 Ofisa Mipango, Catherine Shirima (kulia) wa JICA na Yamae Mikuni kutoka Japan wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Wageni hao pamoja na wenyeji wakiwa katika wodi ya wagonjwa Muhimbili leo.

Na.Agness Moshi-MAELEZO

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekua mkombozi kwa wagonjwa wa moyo Afrika Mashariki kufuatia kupungua kwa gharama za matibabu ukilinganisha na ilivyokua hapo awali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mbunge wa jimbo la Dokolo nchini Uganda Bi.Cecilia Barbara alipotembelea taasisi hiyo ili kuona na kujifunza jinsi Serikali ya Tanzania inavyotoa huduma za Afya kwa wananchi wake .

Bi.Cecilia amesema taasisi hii ni msaada mkubwa kwa Afrika Mashariki kwasababu itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa moyo wanaopelekwa  nchini India au Afrika Kusini kwa matibabu kama ilivyo awali baadala yake watatibiwa Tanzania au nchini kwao.

“Tunahitaji kubadilishana mawazo kama wana Afrika Mashariki, kwasababu kwa kuja hapa tumegundua tunavifaa na uwezo wa kupunguza gharama za matibabu ya moyo“ Alisema Bi.Cecilia.

Bi Cecilia amesema kutokana na ubora huduma zinazotolewa na taasisi hii tangu kuanzishwa kwake serikali ya Uganda imekubali kuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuanzisha mradi kama huu.

“Hatukujua kama Tanzania kuna mradi mkubwa kama huu na unaofanya kazi nzuri lakini kwa kuja tumejua na tunategemea kuanzisha mradi kama huu japo itatuchukua muda kufikia hatua iliyofikiwa na Tanzania”aliongeza Bi.Cecilia .

Naye Afisa Mwandamizi Kitengo cha Utafiti wa Bunge la Uganda Mhe. Jonathan Enamu amesema kuwa amejifunza mengi kwenye ziara hii na ameona ni jinsi gani gharama za matibabu zimepungua kwa wagonjwa wa moyo. “Nimejifunza mengi, ikiwemo jinsi ya kupunguza gharama za matibabu na namna bima za afya zinavyoweza kutumika katika matibabu“ alisema Bw. Enamu.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa , wanatoa huduma kwa watu wote kuanzia daraja la chini na watu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda,comoro,Yemen na Kenya.

Prof.Janabi amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kutumia shilingi bilioni 1.65 badala ya shilingi bilioni 4.72 ambayo ni sawa na kupunguza takribani asilimia 65 ya gharama za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini kama wangewapeleka India kwa matibabu

Prof. Janabi alifafanua kuwa kwa mgonjwa mmoja wa maradhi ya moyo anatibiwa kwa shilingi milioni 35-40 tofauti na nchini India ambapo mgonjwa mmoja anatumia shilingi milioni 120.

Aidha Profesa Janabi ameishukuru Serikali kwa kuipa ushirikiano taasisi hiyo kwani kwa mwaka huu wa fedha Taasisi imepokea asilimia 100 ya bajeti itakayosaidia kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha kuridhisha.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu (MB) amesema kuwa wamewapeleka wageni hao kwenye taasisi ya moyo ili waweze kujifunza na kuona ni jinsi gani Tanzania imefanikiwa kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wa moyo

“wameona namna sisi Tanzania tulivyopunguza gharama kutoka kuwapeleka watu 300 kwa mwaka nje kwa matibabu ya moyo mpaka sasa watu wanne tu, ambao tunawapeleka si kwa sababu hatuna uwezo bali ni kwa sababu ya vifaa havijakidhi “ alisema Mhe.Zungu. 

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ilianzishwa rasmi mwaka 2014 inashughulika na utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wa moyo, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari,ufamasia na uuguzi. Pia taasisi hii inashirikiana na nchi nyingine duniani kwa kubadilishana maarifa,uzoefu na kufanya mafunzo mbalimbali.               

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU