TATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU SEHEMU ZA SIRI NA TIBA- 2TUNAENDELEA na makala yetu kuhusiana na tatizo la kutokwa na uchafu wa rangi mbalimbali sehemu za siri leo tutaeleza na tiba yake, endelea.

Tumeona kwamba mabadiliko ya wingi wa uchafu unaotoka au katika rangi ya uchafu unaotoka ni dalili ya maambukizi ya magonjwa katika uke.

Maambukizi katika uke ni tatizo la kawaida kwa wanawake na wanawake wengi wameshapata tatizo la maambukizi angalau mara moja katika maisha yao.

Ukiona yafuatayo, ujue unaweza kuwa na tatizo la maambukizi ya vijijidudu vya maradhi katika uke wako: Kutokwa a uchafu ukeni kunakoambatana na kuwashwa au vijipele, kutokwa na uchafu ukeni ambako ni endelevu na kwa kiwango kinachozidi kila siku, kusikia maumivu wakati wa kutoa haja ndogo, kutokwa na uchafu mweupe, mzito kama jibini, uchafu wa kijivu/mweupe au njano/kijani unaotoa harufu mbaya.

AINA YA UCHAFU USIO WA KAWAIDA
Kitu chochote kitakachoharibu uwiano wa bacteria wa kawaida waishio katika uke kinaweza
kuleta mabadiliko katika rangi, harufu au muundo wa uchafu utakaotoka katika uke.

Hapa chini naonyesha aina ya uchafu unaotoka, maana yake au chazo chake na dalili ambazo zitatokea kwenye mwili wa mwanamke husika:

Uchafu wenye damu na rangi ya kahawia ni dalili ya mzungumko wa mwezi wa mwanamke uliovurugika na mara chache ni dalili ya kansa ya Cervix au aina nyingine ya kansa iitwayo Endometrial Cancer.

Mwanamke mwenye tatizo hili atatoa damu nyingi ukeni na kuumwa nyonga.

Mwanamke akitokwa na uchafu wenye rangi ya mawingu au njano hiyo ni dalili ya ugonjwa wa kisonono (Gonorrhea). Mwanamke atatokwa na damu katikati ya siku zake, atatokwa na mkojo bila kukusudia na kupata maumivu ya nyonga.

Mwanamke akitokwa na uchafu wa rangi ya kijani ikiambatana na harufu mbaya na ikiwa uchafu utatoka kama mapovu, wenye rangi ya kijani au njano ukiambatana na harufu mbaya, hii ni dalili ya Trichomoniasis, maambukizi (parasitic) yanayotokana na ngono zembe.

Dalili nyigine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.

Ukitoka uchafu mweupe mzito kama maziwa mtindi hiyo ni dalili ya maambukizi ya aina ya fungus (Yeast Infection) na dalili nyingine atakazozisikia mwanamke huyu ni kuvimba na maumivu kwenye sehemu za nje za siri (vulva) na kuwashwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Lakini uchafu ukiwa mweupe au kijivu wenye harufu kama ya samaki hiyo ni dalili za maambukizi ya Bacterial Vaginosis.

Mwanamke mwenye tatizo hili atasikia miwasho au maumivu, kuvimba kwa uke au sehemu ya nje ya uke (vulva).

Maambukizi ya Bacterial Vaginosis, Trichomoniasis na Monilia (Yeast) Infection nitachambua kwa ufupi kila moja na kueleza tiba yake.

Bacterial Vaginosis: Kinachosababisha tatizo hili kitabibu hakifahamiki.

Kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafl a kwa idadi ya bakteria hawa ambao ni kawaida kupatikana kwenye uke na kubadilisha uwiano wao kwenye mazingira ya uke.

Wanawake wenye wapenzi wengi ambao hujamiiana nao au wanaofanya mapenzi kupitia midomo (oral sex) wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya Bacterial Vaginosis.
Dalili za Bacterial Vaginosis ni kuongezeka kwa uchafu unaotoka ukeni kama tulivyosema, kutokwa na uchafu wa kijivu/mweupe, mwepesi au wa majimaji, harufu kama ya samaki ikiambatana na uchafu na harufu inayozidi au uchafu unaozidi mara baada ya kufanya tendo la ndoa.

TIBA YAKE
Tiba kwa tatizo la bacterial vaginosis zipo za aina mbili.

Tiba ya aina ya kwanza ni kutumia dawa iitwayo metronidazole (Flagyl) na tiba ya pili ni kutumia dawa ya kuua bakteria (antibiotic) ya vidonge au ya cream.

Trichomoniasis: Maambukizi haya hutokana na aina ya protozoa wa seli moja. Trichomoniasis mara nyingi huambukizwa kwa kufanya ngono. Protozoa huyu huweza kukaa kwenye mazingira ya unyevunyevu kwa muda wa saa 24 bila kufa hivyo kufanya taulo na nguo nyingine za kuogea kuwa chanzo kingine kikuu cha maambukizi.
Itaendelea wiki ijayo.
Mtaalam A. Mandai
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA