Wana CCM msiojielewa acheni kumkashfu NAPE NNAUYE


Sidhani kama mwana CCM makini anaweza kumkejeli NAPE NNAUYE,
Hebu tumjue NAPE ni Nani ndani ya CCM
Mwaka 2008, NAPE NNAUYE aligundua wizi uliokuwa umesababishwa Na waziri mkuu wa kipindi kile bwana Edward lowassa Na rostam azizi katika ujenzi wa jengo la UVCCM, Na aliwakomalia sana mpaka NAPE NNAUYE akatishiwa maisha yake, hadi mwenyekiti wa chama jakaya kikwete akatishia kumnyanganya kadi, na kwa wanaojua sakata ili tafuta habari za mwaka 2008 , NAPE alitawala vyombo vya habari,
2009 akiwa Na samweli sitta marehem sasa, baada ya kuona mwenendo wa CCM si mzuri kwa kukumbatia wala rushwa Na mwenyekiti hakuwa Na la kusema ikabidi watishie kuanzisha chama kingine, yaan CCJ, Na wakajiandaa kusimamisha mgombea, lakin ikachezwa mizengwe kutosajiri chama kile maana mamlaka zote alizuia kikwete, mbona mnakuwa wasahaulifu hivi?
Huyu huyu NAPE NNAUYE ndo amesimamia kuvua gamba Na kupigia kelele Jambo la kujivua gamba mwaka 2010 mpaka rostam azizi akaachia ngazi, Leo hii mnamkejeli NAPE,
NAPE NNAUYE mwaka 2013 amezunguka nchi nzima Na mheshimiwa Abdulrahman Kinana kuitangaza CCM Na kuitaka serikali kuwajibisha mawaziri mizigo, Leo hii mnamkataa NAPE NNAUYE??
NAPE NNAUYE kapokonywa ushindi wake wa kugombea ubungo, ikabidi vijana wamuunge mkono mnyika, kikwete ikabidi ampe ukuu wa wilaya MASASI kupunguza munkari, Leo hamumjuhi NAPE NNAUYE??
NAPE NNAUYE kamkataa lowassa waziwazi Na kumuaibisha kwenye vyombo vya habari kumbu kumbu zipo ,kwenye mchakato wa kutafta wagombea, Na alisema " PANYA AKIINGIA KWENYE MTUNGI USIVUNJE MTUNGI ,INAMISHA ATOKE UMUUE" aliyasema hayo clouds FM, Leo hamumjuhi NAPE NNAUYE??
NAPE NNAUYE ndo kapata ajari akihamasisha upigaji kura mwaka 2015 Leo hii mnamkejeli NAPE NNAUYE
Acheni kumuandama NAPE NNAUYE,
By raia mpenda haki
LikeShow more reactions
Comment
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA