WAZIRI KAIRUKI AANZA ZIARA DAR

Waziri Ofis ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angelah Kairuki akizungumza na  Meya wa Temeke, Abdalah Chaurembo pamoja na Katibu Tawala wa wilaya ya Temeke, Hashim Kambi alipoanza zira ya kikazi wilayani humo jana.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angelah Kairuki akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Felix Lyaniva wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kutembelea wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam jana. (PICHA NA DALILA SHARIF)

Na Dalila Sharif
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, ameanza ziara yake Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo kuzifahamu changamoto mbalimbali za watumishi na kutoa maelekezo ya kutatua kero hizo kwa ajili ya kuboresha maslahi ya ufanyakazi bora.

Katika ziara yake ambayo ameanza na Wilaya ya Temeke Waziri Kairuki ameagiza uanzishwaji wa vituo vya kusaidia upatikanaji wa huduma kwa wakati maarufu kama 'One Stop Center' katika  idara ya Mamlaka ya Mapato (TRA) na idara ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ili kuongeza ufanisi wa kazi na ukusanyaji wa kodi kwa wakati, halkadhalika uwepo usajili wa biashara kwa haraka ambapo itasaidia katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Tanzania kwa watanzania wanyonge.

"Hizi One Stop Center ni muhimu sana baadhi ya Mikoa imeanza kunufaika na uanzishwaji wake ikiwemo Mkoa wa Morogoro ambapo imepelekea ukusanywaji wa mapato kwa haraka na kuchochea shughuli za maendeleo" alisema Waziri Kairuki.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ametoa msisitizo kwa Maafisa Utumishi kuhakikisha serikali inapotoa vibali vya kazi, hawaajiri watu bila kujiridhisha na taarifa zao za kielimu ili kuepuka suala la watumishi wenye vyeti feki, ambapo ameeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyowakilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Michael Mungaya wa Mkoa wa Dar es Salaam imeeleza kuwa watumishi 937 wanavyeti feki na katika hao 421 wameleta vyeti pungufu, ni vyema umakini  ukafanyika ili kuondoa hasara kwa taifa.

Waziri Kairuki ameongeza kuwa  mfumo wa taarifa za watumishi (Lawson) utasaidia katika kuhakiki taarifa zao ikiwemo kujua mahala walipo watumishi  na wanafanya nini, hivyo kupitia mfumo huo watajiridhisha na kufanya maamuzi sahihi kwa watumishi.

Aidha Waziri Kairuki amewasihi watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi bila ya ubaguzi wa aina yeyote na kutenda haki kwa kufanya kazi kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, halikadhalika kuepuka suala la kutoa au kupokea rushwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amemuomba Waziri Kairuki kuhakikisha kuwa watumishi wanapewa makazi jirani na vituo vyao vya kazi ili kuboresha ufanisi kazi na uwepo wa usalama na ulinzi, pia DC Lyaniva amemueleza Waziri Kairuki kuwa wameweza kuongeza saa limoja la ziada la kuwahudumia wananchi katika wiki ya utumishi wa umma iliyofanyika tarehe 16 mpaka 23 mwezi June.

Pia Lyaniva alisema tayari ameshawambia  watumishi wa wilaya hiyo kuacha kufanyakazi kwa mazoea hali hiyo itasaidia kutoa huduma kwa wakati na weledi katika kuwajibikia wananchi.
mwisho...

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI