BARCELONA YAANZA VIZURI LA LIGA BILA SUAREZ NA NEYMAR YAITANDIKA REAL BETIS


Wakicheza bila ya mshambuliaji wao hatari Neymr amabye amehamia PSG pamoja na Luis Suarez aliye na majeruhi timu ya Barcelona imeanza vyema katika kusaka taji la Ligi Kuu ya Hispania kwa kupata ushindi wa magoli 2-0 katika mechi yake ya La Liga dhidi ya Real Betis.
Wakicheza kwa kujiamini licha ya kufungwa na mahasimu wao wakubwa Real Madrid katika mchezo wa Ngao ya Hisani walipata magoli yao kupitia kwa Alin Tosco aliyejifunga dakika ya 36 huku beki Sergio Roberto akipingilia msumari wa pili dakika ya 39.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuwasaidia Real Betis hadi dakika 90 Barcelona wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0 na pointi tatu muhimu.
Katika Uwanja wa Camp Nou, kulikuwa na ulinzi wa ziada kutokana na shambulio la kigaidi lililotokea siku tatu zilizopita na kusababisha vifo vya watu 14.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI