4x4

BREAKING NEWS: POLISI DAR WAUA JAMBAZI MMOJA, WENGINE WATIWA MBARONIKamanda Mkondya.
JESHI la Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam limemkamata mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi katika msako ambao umefanyika hiyo karibuni maeneo ya Vijibweni.

Akitoa taarifa hiyo mapema leo Agosti 11, 2017, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar, Lucas Mkondyaamesema kuwa jambazi huyo alikamatwa akiwa nyumbani kwake.

“Tulimkamata mmoja ambaye alitupeleka mpaka kwa nyumbani kwa huyo mwenzake, alipotuona tupo na jamaa yake akaingia ndani aakarudi na bastola. Lakini kabla hajatushambulia maaskari walimuwahi wakampiga risasi ya bega, tukampokonya silaha. Alianza kuvuja damu nyini tukampeleka Hospitali ya Vijibweni lakini bahati mbaya alifariki,” alisema Kamanda Mkondya.

Aidha kamanda mkonya ameeleza kuwa jeshi hilo limefanikiwa kukamata magunia ya bangi, kete zinazozaniwa kuwa ni za dawa za kulevya pamoja na mtandao wa wezi wa magari jijini hapa ambapo watuhumiwa wote bado wanaendelea kuhojiwa na mara tu upelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.


MSIKIE KAMANDA AKIFUNGUKA
Post a Comment