DAU LA KWANZA LA USAJILI LA MSUVA LILIKUWA LAKI MBILI, LOTE LILITOLEWA SADAKA KANISANI




Baba mzazi wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Saimon Msuva amesema fedha yote ya usajili ya kwanza kabisa ya mwanaye waliipeleka kanisani na kufanya maombi.

Happygod Msuva amesema walifanya hivyo baada ya Msuva kulipwa Sh 200,000 na Moro United kama usajili wake.

“Baada ya kulipwa, tulichukua dau lote la usajili la Sh laki mbili alizokuwa amepewa. Tukaenda kanisani na kutoa sadaka yote, pia tutafanya maombi.

“Pamoja na juhudi kubwa anazofanya yeye pamoja na familia lakini tumekuwa tukifanya maombi, tunamuomba Mungu na kweli njia  tumekuwa tukiiona,” alisema.

Happygod ambaye ni fundi maarufu wa magari katika eneo la Mabibo, amesema anaamini mwanaye atapiga hatua zaidi kwa kuwa ni mtu anayetaka mafanikio.

Kwa sasa Msuva anakipiga katika kikosi cha Difaa Al Jadid cha Morocco.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU