Everton yaivuta shati Man City nyumbani


EPLHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWayne Rooney amefikisha jumla ya magoli 200 katika ligi kuu ya nchini England
Matajiri wa jiji la Manchester klabu ya Man city,imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Everton.
Everton almaarufu kama The Toffes, ndio walianza kuzifumania nyavu za Man City, kwa goli lilifungwa na mshambuliaji Wayne Rooney, Rooney amefikisha idadi ya magoli 200 katika michezo ya ligi kuu nchini England.
Katika dakika ya 82 Man City, walisawazisha goli hilo kupitia kwa winga Raheem Sterling aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Everton, Jordan Pickford.
EPLHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRaheem Sterling akipiga shuti lililokwenda moja kwa moja nyavuni
Mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kubakia na wachezaji kumi baada ya beki wa City Kyle Walker, na kiungo wa Everton Morgan Schneiderlin, kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kila mmoja kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA