JAFO AWAHAMASISHA WATUMISHI SINGIDA KUJENGA UPENDO


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Singida katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Singida.
....................................................................
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewahamasisha watumishi wa halmashauri ya wilaya Singida kufanyakazi kwa bidii pamoja na kujenga upendo baina yao. 

Jafo ametoa kauli hiyo leo asubuhi alipokuwa akipita akitokea katika ziara ya kikazi mkoani Mara.

Akiwa mkoani humo, Jafo amesimama kwa muda mfupi wilayani hapo ili awasalimie na kuwatia moyo katika utumishi wao. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida Rashidi Mohamed Mandoa amemshukuru Naibu Waziri Jafo kwa upendo wake wa kusimama wilayani hapo na kukutana na watumishi.


“Kitendo hichi kinawapa hamasa kubwa watumishi kwa kuona kwamba wanathaminiwa na viongozi wao,”amesema Mkurugenzi huyo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI