JE KOREA KASKAZINI KUWA DAUDI DHIDI YA GOLIATI?




(Pichani: Moja ya ndege za hatari za Marekani B1)
Mwaka 2009 Marekani Ilipiga bomu kubwa sana mwezini katika harakati za kuuchimba mwezi kutafiti uwepo wa maji, Tar 5, August 2011 Marekani katika moja ya safari zake nyingi za anga za mbali ilirusha chombo wanachokiita “JUNO” kiende Sayari ya Jupiter ambapo kilisafiri kwa miaka 4 Miezi 10 na siku 29 na kuwasili katika paa la sayari Jupita Tar 5 July 2016. Chombo hicho chenye uwezo wa mwendo kasi kati ya 126,000 hadi 150,000 Km kwa saa, sawa na umbali wa Dar-Mwanza zaidi ya Mara 100 kwa sasa kinaleta picha na taarifa mbali mbali za sayari hiyo.
Katika medani za kivita idadi ya ndege zote za jeshi la China (2,955) ukizujumlisha na zote za Jeshi la Urusi (3,793) hazifiki nusu ya idadi ya ndege za jeshi la Marekani (13,762) huku ndege zake za aina tatu B1, B2 na B52 ambazo wanazo lukuki inaelezwa ndege moja tu katika ndege za muundo huo yaani B1 moja tu, au B2 moja tu au b52 moja tu kama inaamrishwa kufanya mashambulizi ya kiwango chake cha juu kabisa inaweza kuimaliza Korea Kaskazini yenye ukubwa wa maili 46.5 za mraba ikiwa na watu milioni 25 kwa dk 15 tu ila ndio mamilioni ya watu wataangamia. Wakati huo huo Jumla ya Ndege zote za Korea Kaskazini ni 944.
Bajeti ya ulinzi ya Marekani (Dola bilioni 587.8) ni mara 78 ya bajeti ya Korea Kaskazini (Dola bilioni 7.5) , zaidi ya mara 13.1 ya bajeti ya Urusi (Dola bilioni 44.6), zaidi ya Mara 3.6 ya bajeti ya Ulinzi ya China (Dola bilioni 161.7). Wakati duniani hakuna nchi nyingine yenye manoari zenye uwanja wa ndege za kivita zinazofikia tatu, Marekani yenyewe inazo 12 na zenye uwezo mkubwa kiteknolojia. Aidha meli za kawaida za mashambulizi nyingi zina uwezo wa kurusha makombora 60 ya masafa marefu aina ya Tomahawk kwa dakika 5 tu, fahamu kombora moja lina ukubwa na uzito wa tani moja na nusu.
Hivi karibuni hali imezidi kuwa tete baada ya Korea kuwekewa vikwazo vikali zaidi vya kiuchumi ambapo wakaitangazia dunia Kwamba watalipiza kisasi vikali kwa Marekani, siku chache baada ya kauli hiyo ya Korea Kaskazini Satellite za Marekani zimegundua Korea Kaskazini wapo kwenye harakati za kutayarisha majaribio mengine mawili ya makombora na wanastawisha nuclear zao ndipo Rais Donal J. Trump akaiambia Korea isiendelee kuitishia Marekani itakutana na Moto na Gadhabu, itapewa kipigo ambacho dunia haijawahi kukishuhudia. Baada ya kauli hiyo ya Trump Korea wakajibu kwamba wanakusudia kushambulia kisiwa cha Guam. Guam ni kisiwa kilichopo katika bahari ya Pasifiki chenye moja ya kambi kubwa za jeshi la Marekani ambacho pia kina wakazi 162,000.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis ambaye pia anajulikana kwa majina ya Warrior Monk, Mad Dog na Chaos amerudia kutoa onyo kali kwa Korea Kaskazini na kusema wanachotaka kukifanya Korea kitasababisha utawala wa nchi hiyo kuondolewa pamoja na maangamizi kwa watu wake. Baada ya Kauli hiyo Korea Kaskazini imetangaza inajitayarisha kurusha makomboa manne kuelekea kisiwa cha Guam lakini ikikusudia yatue kilometa 30 au 40 kabla ya kisiwa chenyewe hatua hiyo inayokusudiwa kutekelezwa siku chache zijazo ni onyo kwa Marekani.
JE KOREA KASKAZINI ATAFAULU KUWA DAUDI DHIDI YA GOLIATI? Nini Mtazamo wako.
Taarifa na uchambuzi umeletwa kwenu Na Jacob Malihoja kwa hisani ya Mitandao mbali mbali www.google.com, www.nasa.gov,www.globalfirepower.com, www.wikipedia.org. www.rt.com, www.bbc.com,www.cnn.com, www.foxnews.com, www.youtube.com etc.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*