JPM AAMURU MGAMBO JKT KURUDISHA ENEO LA EKARI 50


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameamuru eneo la ekari 50 lililopo Mkata mkoani Tanga ambalo walipewa Mgambo JKT miaka saba iliyopita kwa ajili ya kujenga kiwanda na wakashindwa kuliendeleza, walirudishe haraka kwa serikali ya kijiji ili lipangiwe matumizi mengine.

Hayo ameyasema leo wakati akiwa njiani kuelekea Tanga kwa ajili ya kumpokea mgeni wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ambapo kesho wataweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Kaskazini mwa Tanga.

Rais Magufuli amekuwa akisisitiza kuwa wawekezaji au taasisi itakayopewa eneo kwa ajili ya kujenga kiwanda lazima ifanye hivyo, kushikilia eneo bila kuliendeleza kutasababisha mhusika anyang’anywe eneo hilo na apewe mwingine mwenye uwezo wa kuliendeleza.

Aidha rais ametoa onyo kwa viongozi waliohusika kuhujumu kwa kujinufaisha na fedha kiasi cha Tsh milioni 500 za ujenzi wa Hospitali ya Mkata kuwa wajiandae kuzirudisha ama kwenda gerezani.

: Mabomba ya maji yameshatandazwa hapa mkata, matenki yatawekwa, lazima tuhakikishe maji yanapatikana. @MagufuliJP
: Waliohusika kujinufaisha na fedha mil. 500 za ujenzi wa hospitali wajiandae kuzirudisha au kwenda gerezani. @MagufuliJP
: Eneo la ekari 50 walilopewa Mgambo JKT na serikali ya kijiji miaka 7 iliyopita ili wajenge kiwanda wakashindwa, walirudishe.

MTAZAME RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA HAPA0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR