KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA



                   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
OFISI YA KAMISHNA JENERALI
 JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
  S. L. P. 5821,
  DAR ES SALAAM.
 


Simu ya maandishi: “ZIMAMOTO KUU”
Simu Nambari:  +255-22-2181093
Telefax:          + 255-22-2184569
Barua Pepe: fire.rescue@frf.go.tz


 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vitengo wa Jeshi hilo.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi (ACF) Bakari Mrisho, amekuwa Mkuu wa Chuo na Mafunzo, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu (SF) Kennedy Komba, ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Iringa na nafasi yake inachukiliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) James John toka Makao Makuu.
Kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi (ACF) Gilbert Mvungi, amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Baraza Mvano ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma.
Kamanda wa Viwanja vya Ndege  Nchini, Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Kwiyamba amehamishiwa Makao Makuu, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Christom Manyologa.
Kamishna Msaidizi (ACF) Fikiri Salla amekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, anajaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto.
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Mrakibu Msaidizi (ASF) Goodluck Zelote amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Tanga, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Happy Shirima toka Makao Makuu.
Mrakibu Msaidizi (ASF) Fatma Ngenya amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Mkaguzi Msaidizi (A/INSP) Heriel Kimaro ambaye amehamishiwa Makao Makuu.
Uhamisho huo ni Mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.  
 Imetolewa na;
KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA,
MAKAO MAKUU.

16 AGOSTI, 2017.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI