NANENANE IWE NA FAIDA INAYOONEKANA KWA MKULIMA, MFUGAJI NA KILA MSHIRIKI- DKT NCHIMBI


Maonyesho ya nane nane yanatakiwa kuweka alama chanya na kuwa na sura ya mabadiliko yanayoonekana kwa macho kwa wakulima na wafugaji wanaoshiriki pamoja na wananchi wanaopata huduma na bidhaa katika maonyesho hayo.

Mgeni rasmi katika Ufunguzi wa maadhimisho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Chimbi ametoa rai hiyo mapema jana kwa wakulima, wafugaji na washiriki wakati akifungua rasmi maonyesho hayo huku akiwataka washiriki hao kuitumia fursa hiyo kwa manufaa zaidi.

“Ni vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa washiriki mliojitokeza katika kuonesha bidhaa zenu mbalimbali na pia kwa wale wote waliofika kwaajili ya kununua au kupata maelezo ya matumizi ya bidhaa hizo, wapate kitu tofauti kitakachooneka katika maisha yao”, amesema.

Dkt Rehema Nchimbi ambaye ametumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo na ufugaji wenye tija ili kuendana na falsafa ya serikali ya awamu ya Tano inayo himiza zaidi Uchumi wa Viwanda.

Aidha ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani na nje ya Nchi wafike kuwekeza katika mikoa ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa kila atakayekuwa tayari kuwekeza katika Mikoa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionja asali katika moja ya mabanda ya maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama bidhaa za mbogamboga katika banda la Wilaya ya Kondoa katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mkoa wa Singida katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionyeshwa shamba la mahindi lilostawi vizuri katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Julius Sang’udi alipotembea banda la jeshi la magereza kujionea bidhaa wanazotengeza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoka katika banda la Tume ya taifa ya Umwagiliaji, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma. 
Picha kwa hisani ya domhabari24.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.