RAIS MAGUFULI AMALIZA BIFU LA MAKONDA NA RUGE JUKWAANI

Paul Makonda akishikana mkono na Ruge Mutahaba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amemaliza bifu kubwa lililokuwepo kati ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuwakutanisha wawili hao jukwaani na kuwataka washikane mikono.
Tukio hilo la aina yake, limetokea leo AGOSTI 5, 2017 kwenye Kijiji cha Chongoleani, Tanga ambapo kulikuwa na tukio kubwa la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda mpaka kwenye Bandari ya Tanga.

Tazama Ruge na Makonda Wakicheza Muziki Baada ya Kupatanishwa na Rais Magufuli

Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Ruge kwa kazi nzuri anayofanya, ikiwemo kampeni yake ya Ishi na Mimi inayoendeshwa na Clouds Media na kuwakutanisha wasanii wote wakubwa kwenye jukwaa moja kuimba nyimbo za kizalendo.

Rais Magufuli Alivyomaliza Bifu la Makonda na Ruge


Akawataka wawili hao, kwa kuwa wote ni vijana, wamalize tofauti zao na kuchapa kazi kwa bidii kwani anawapenda wote wawili, kitendo kilichoibua shangwe kubwa kwa watu waliokuwepo kwenye tukio hilo.
Chanzo cha ugomvi wa wawili hao, yalikuwa ni madai ya Makonda kuvamia kwenye ofisi za Clouds FM akiwa na askari wenye silaha, akidaiwa kushinikiza kipindi alichokuwa na maslahi nacho kirushwe hewani, jambo lililosababisha vuguvugu kubwa miongoni mwa waandishi wa habari na wananchi kwa jumla.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)