SPORTPESA WAMUALIKA SOL CAMPBELL, BEKI HUYO KISIKI WA ZAMANI WA ARSENAL AMEKUBALI, ANAKUJA TANZANIA


Vichwa vya watanzania bado vina masalia ya ziara ya Wayne Rooney na Everton yake kwani ukiingia kwenye mitandao ya kijamii bado mazungumzo hayajaisha kutokana na ukweli kuwa ziara ile ilikuwa na uzito mkubwa na ya kipekee katika historia ya tasnia ya michezo nchini.

Kuna watu walipata nafasi ya kutimiza ndoto zao za kukutana na mastaa mbalimbali wanaocheza EPL, ikiwa ni ligi inayotazamwa zaidi Ulimwenguni na hata kupata nafasi ya kupiga nao picha huku Rooney akiwa ndio kivutio kikubwa huku haya yote yakiwezeshwa kwa udhamini mkubwa wa SportPesa.

Wakati mang’amung’amu hayo ya ujio wa Everton yakiwa bado vichwani mwa mashabiki wa soka, tayari kuna taarifa ya ujio mwingine mkubwa nchini kwa udhamini wa SportPesa.

Ikiutumia vyema ushirika wake na vilabu vya EPL, SportPesa sasa inamleta nguli na balozi wa klabu ya Arsenal kutoka jijini London ambao ni mabingwa mara 13 wa Ligi Kuu ya Uingereza huku pia wakiwa ni mabingwa wa kihistoria wa kombe la FA ambao wamelitwaa mara 13.


Mkataba
Ujio wa Sol Campbell nchini Agosti 5 mwaka huu ni mwanzo wa ushirika kati ya klabu ya Arsenal na Tanzania kupitia kampuni ya SportPesa ambao ni washirika rasmi wa Arsenal katika michezo ya kubashiri kwa bara la Afrika.

Arsenal na SportPesa waliingia mkataba wa miaka mitatu na nusu ambao utaishuhudia klabu hiyo ya Arsenal ikileta maofisa wake wa benchi la ufundi kwa ajili ya kuendesha kliniki za soka kwa makocha na wachezaji barani Afrika na tayari wameshafanya hivyo mara kadhaa nchini Kenya.


Ujio wa Campbell
Atakapokuwa nchini, Sol Campbell atapata nafasi ya kutembelea klabu ya michezo ya walemavu ya Muungano na kubadilishana nao mawazo na kisha siku ya tarehe sita pia atatembelea shule ya soka ya Magnet katika viwanja vya Gymkhana ambapo atapata nafasi ya kukutana na wachezaji chipukizi, kucheza nao na pia kuwapa hamasa katika safari yao ya soka.

Kubwa zaidi ni pale ambapo Campbell ataongoza jopo la wapenzi wa klabu ya Arsenal nchini kutazama mechi ya Ngao ya Hisani siku ya Jumapili ya Agosti 6 kati ya klabu ya Arsenal ambao ni mabingwa wa FA dhidi ya Chelsea ambao ni mabingwa wa EPL.

Hakika itakuwa ni fursa adhimu kwa wapenzi wa mpira nchini hususani wale wa Arsenal kukutana na nyota wao huyo wa zamani, kuongea na kupiga nae picha ikiwa ni ndoto ya kila shabiki wa soka duniani kukutana na nyota anayemkubali.

Ikumbukwe kuwa Arsenal ni klabu inayoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Tanzania hali kadhalika barani Afrika. Hivyo naona jinsi ambavyo ujio huu wa Sol Campbell unavyotimiza ndoto za kundi kubwa la mashabiki wa soka nchini. Upo tayari?


Campbell ni nani?
Sol Campbell alijiunga na Arsenal mwaka 2001 akitokea klabu ya Tottenham Hotspurs ambaye aliiongoza safu ya ulinzi ya klabu ya Arsenal kucheza mechi 49 bila kufungwa huku pia wakiweza kutwaa ubingwa wa EPL kwa msimu wa 2003-2004.

Campbell aliondoka Arsenal mwaka 2006 na kujiunga na Portsmouth na nchini Uingereza pia kabla ya kurudi klabu ya Arsenal kwa mara ya pili mwaka 2009 baada ya walinzi William Gallas na Thomas Vermalen kuumia.


Campbell aliondoka Arsenal mwaka uliofuata na kutimkia Newcastle United ambapo alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Mei mwaka 2012, Campbell alistaafu rasmi kucheza soka. Campbell ameichezea Arsenal mechi zaidi ya 200 na kufunga magoli 12 katika vipindi vyote viwili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI