TFF YATOA MSISITIZO KWA KLABU KUHUSIANA NA USAJILI WA MTANDAONIWakati zimebaki siku nne (4) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kwa msimu wa 2017/18, tunazikumbusha klabu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na 24 Ligi Daraja la Pili kukamilisha usajili kwa Mfumo wa Mtandao wa TMS – Transfer Matching System.
Ikumbukwe kuwa dirisha la usajili linafungwa Agosti 6, mwaka huu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatoa angalizo kwamba hakuna klabu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kama haitapata leseni ya klabu.
Baadhi ya klabu hazijachukua hata fomu za leseni ya klabu wakati zile zilizochukua kuna baadhi hazijarejesha na pamoja kwamba kuna zile ambazo zimerejesha, lakini baadhi inaonekana hazikujazwa kwa usahihi.
Kikao cha Kamati ya Leseni za Klabu, chini ya Msomi Wakili Lloyd Nchunga kinatarajiwa kuketi Jumamosi Agosti 5, mwaka huu kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambako kitapitia fomu zilizorejeshwa kabla ya kufanya uamuzi wa kutoa leseni kwa klabu zilizotimiza masharti.
Klabu ambayo haitapata leseni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), haitakuwa na nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2017/18.
Suala la leseni linakwenda pia kwa wachezaji. Kama ilivyokwisha kutangazwa, hakuna mchezaji atakayeshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili - michuano inayoendeshwa na kusimamiwa na TFF kama hakutimiza masharti ya kupata leseni ya kumruhusu kucheza.
Kuna vigezo sita (6) vya mchezaji kupata leseni ambavyo ni: -
1. Kujazwa fomu ua utimamu wa afya (Medical Form).
2. Bima ya matibabu kwa mchezaji.
3. Barua ya uhamisho (Release Letter).
4. Hati ya Uhamisho wa Kimataifa kwa wachezaji wa kigeni.
5. Mikataba ya wachezaji iliyosajiliwa kwenye mfumo wa usajili TMS
6. Ada ya wachezaji wa kigeni ambayo ni Sh 2,000,000 badala ya dola 2,000 za Marekani.

Wakati hayo yakiagizwa, maandalizi ya ujio mpya wa msimu wa mashindano yanaendelea ambako kwa kesho Alhamisi, Agosti 3, mwaka huu Kampuni ya Vodacom - inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano nchini Tanzania itatoa vifaa vya mchezo kwa timu zote 16 za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa ndiyo Mdhamini Mkuu wa michuano hiyo yenye ushindani mkali. Vodacom wanafanya hivyo kwa mujibu wa mkataba wa udhamini.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.