UVCCM MKOA WA IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI WATAKA MAFISADI KUJIONDOA WENYEWE



Viongozi wa UVCCM mkoa  wa Iringa  wakiunga mkono utendaji kazi wa Rais Dkt  John Magufuli  leo   baada ya kumalizika kwa zoezi la kutoa tamko la kumpongeza Rais kwa kazi nzuri ,kutoka  kulia ni mkuu wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah ,katibu  UVCCM Iringa mjini Alophonce Munyinga , mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza , katibu UVCCM mkoa James Mgego , katibu UVCCM  Iringa  vijiji  Ignas Kinyowa na  viongozi  wengine

Vijana walioshiriki zoezi hilo 
Vijana wa UVCCM wakiwa katika zoezi hilo la kumpongeza Rais Dkt Magufuli
Vijana  wakiajiandaa kutoa tamko lao leo 
Katibu  wa UVCCM mkoa  wa Iringa James Mgego  katikati  akiwa na makatibu  wake  wa  wilaya kushoto ni katibu wa Iringa mjini Alophonce Munyinga  na kulia ni katibu wa UVCCM Iringa  vijijini Ignas Kinyowa 
Na  MatukiodaimaBlog
UMOJA  wa vijana wa  chama  cha mapinduzi (UVCCM)  mkoa  wa Iringa  umepongeza  hatua ya  Rais  Dkt  John Magufuli kutengua  uteuzi  wa aliyekuwa  waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter   Muhongo  baada ya  ripoti ya uchunguzi wa mchanga  wa dhahabu  na kataka  mawaziri  zaidi  watakaohusishwa na  ufisadi   kutumbuliwa .

Huku  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza akidai  kuwa mkoa wake  hauzui wananchi kumpongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia ila hatapenda  kuona  wananchi  wanaunga mkono maamuzi mbali mbali ya  Rais kwa kufanya vurugu na kuandamana barabarani .

Akizungumza na  wanahabari  leo ofisini kwake juu ya tamko  hilo la  kumpongeza Rais Dkt  Magufuli kwa kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa James  Mgego alisema vijana  mkoani  hapa  wamepokea kwa  mikono  miwili uamuzi  huo wa  Rais wa  kumuondoa waziri Prof  Muhongo  na  kutaka  mawaziri na viongozi  wengine wa  umma kuwajibika kwa faida ya umma na si vinginevyo.

“ Umoja  wa vijana mkoa wa Iringa unaungana na kaimu katibu mkuu wa  UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka  kupongeza hatua  iliyochukuliwa na Rais wa  jamhuri ya muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM Taifa  Dkt  John Pombe Magufuli  kwa hatua  alizozichukua  za kizalendo  kwa maslahi ya watanzania  kwa  kutengua  uteuzi wa waziri wa Nishati na madini ….Rais amefanya  jambo zuri  ambalo  linapongezwa na kila mtanzania kwa faida  ya  vizazi  vilivyopo na vijavyo “
Alisema kuwa Rais Dkt Magufuli  amechukua uamuzi sahihi  wakati  sahihi  kwani nchi  ilikuwa  ikipoteza raslimali  nyingi kwa  ajili ya kuwanufaisha  wachache  kwa maslahi  yao  wenyewe na sio jamii ya kitanzania .

Hivyo alisema kuwa  umoja wa  vijana  wa CCM mkoa wa Iringa  umeona ni  vema kujitokeza  mbele ya  vyombo  vya habari  kupinga vikali  vitendo vya rushwa na ufisadi ,dhuruma na  wizi  vinavyofanywa na baadhi ya  viongozi  wasio  wazalendo na Taifa  .

Mgego  alisema UVCCM mkoa wa Iringa haitasita kuwafichua  wale  wote  ambao  wanaikwamisha  serikali kwa  kufanya vitendo vya ufisadi ama  dhuruma  dhidi ya  watanzania  kwa  kutumia nafasi  zao  za  uongozi walizo  pewa .
Aidha  alisema  kwa kuwa  ripoti ya  pili  ya kiuchunguzi  dhidi ya mchanga huo wa madini inakuja ni  vizuri  wale  wote  waliohusika kwa namna moja ama nyingine  kujitafakari na  kuchukua hatua ya  kujiuzulu nafasi  walizopewa kabla ya  kutumbuliwa na Rais .

Pia katibu  huyo  aliwataka vijana  kuendelea kujitokeza  kuchukua  fomu  za kuwania nafasi mbali mbali ndani ya chama  hicho na  kutowasikiliza  mafisadi  ambao  wapo  kuona  CCM inakwama katika  uchaguzi  huo wa ndani ya  chama .
Katibu  wa UVCCM wilaya ya Iringa mjini Alphonce Muyinga  alisema kuwa wanazo taarifa  za  wote  wanaohujumu  uchaguzi wa CCM mkoani Iringa na kuwa dawa yao inachemka  kwani  hawataona  haya  kuwashugulikia watu hao  wanaotaka kukwamisha uchaguzi  huo wa CCM .

Mkuu wa  mkoa wa Iringa  Masenza ambae  alialikwa katika  zoezi hilo la utoaji wa tamko alipongeza  hatua  ya  vijana  hao kutambua kazi  kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli na hata  kutoa tamko  hilo la pongezi .

Masenza  alisema kuwa kumekuwepo na maombi kutoka kwa wananchi wa kawaida maeneo mbali mbali ya mkoa wa Iringa  kuomba kufanya maandamano makubwa ya  kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na maamuzi mbali mbali yenye lengo la  kuwakomboa  watanzania  na kuwa hakuna kiongozi anaye zuia  wao  kukutana kutoa pongezi  zao  kwa Rais ila si kwa  kuandamana mitaani .

“ Mimi kama mkuu wa mkoa wa Iringa nawapongeza  pia wananchi wangu ambao wametambua kazi nzuri inayofanywa na Rais   wetu katika Taifa ….nawaomba sana wananchi wenye  pongezi kwa rais ruksa  kuzitoa ila utaratibu  ambao wanapaswa  kuutumia ni  kukutana katika  vikao  vya ndani kama  walivyofanya  vijana wa CCM na sio  kufanya maandamano mitaani”

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI