MKIKITA SASA YAINGIA KWENYE MPANGO WA MIAKA MITANO YA MAENDELEO

 Mtaalamu wa Masoko wa Kimataifa kutoka Ufilipino, Dk. Muni akitoa somo kuhusu umuhimu wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuwa na Mpango wa miaka miatano wa maendeleo wakati wa mafunzo kwa wafanyakazi wa mtandao huo  yaliyofanyika Makao Makuu ya Mkikita, Dar es Salaam. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


Na Richard Mwaikenda
MTANDAO wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), umeandaa Mpango Mkakati wa Maendeleo wa Miaka mitano kwa lengo la kung'aa kiutendaji ndani na nje ya nchi.

Mpango huo umeandaliwa kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa mtandao yaliyoendeshwa na Mtaalam wa Masoko kutoka Ufilipino, Dk. Muni ambaye yupo nchini kwa mwaliko wa mtadandao huo.

Katika Mafunzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu ya Mkikita, Dar es Salaam, Dk. Muni aliwafundisha kuhusu umuhimu wa Mtandao huo kuwa na Vision na Mission.

Alisema kuwa Mkikita bila kuwa na Vision na Mission hauwezi kupata mafanikio, hivyo ni muhimu wafanyakazi na menejimenti kuwa kitu kimoja kufanikisha mpango huo.

Alitaja mambo muhimu yanayopaswa kuwemo kwenye vision kuwa ni; kuazimia kuwa mtandao wa kimataifa, kuongozaa wanachama, kuongeza ajira kwa vijana, kuongeza uzalishaji na masoko, kuwa na miradi mbalimbali.

Pia kwa upande wa Mission, Dk. Muni  alisema Mkikita inatakiwa kwa mFumo mzuri wa Uendeshaji,  kuwa na Menejimenti na Wafanyakazi wenye bidii ya kufanya kazi, kuwepo uwazi na ukweli, udhibiti mzuri wa fedha, huduma nzuri kwa wateja pamoja na mpango mzuri wa maendeleo.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa pia na Wakurugenzi wa bodi ya Mkikita wakiongozwa na Dk. Kissui Steven Kissui pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Adam Ngamange.

Dk. Kissui alisema kuwa wameamua kuandaa mafunzo hayo kwa wakurugenzi na wafanyakazi wote ili  wawe kitu kimoja katika kufanikisha azma yao ya kuhahikisha mtandao huo unapiga hatua za haraka za maendeleo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akiwataka wafanyakazi na menejimenti kufanya kai kwa umoja na bidii ili kuufikisha mtandao huo mbele zaidi kimaendeleo
 Dk. Muni akipongezana na Dk Kissui
 maandalizi ya mafunzo hayo

 Mfanyakazi wa Mkikita, Happy akizungumza wakati wa mafunzo hayo
 Dk. Muniakielezea umuhimu wa Mtandao huo kuwa nA Vision. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui


 Dk. Muni akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
 Suchakk akiwataka wafanyakazi kuacha kuwa na aibu wanpoamua kufanya jambo muhimu
 Mhasibu Mkuu wa Mkikita, Mshashu akielezea jinsi ya kuboresha kitengo cha uhasibu
 Mkurugenzi Mtendaji wa MKIKITA, Adam Ngamage

 Dk. Kissui akitoa neno la shrani kwa mafunzo hayo na kusisitiza kuwa na utendajiwa pamoja kati ya menejimenti na wafanyakazi


 Sasa ni wakati wa kuchapa kazi. Ndivyo Dk. Kissui alivyoweleza wafanyakazi
Suchakk akipongezana na Dk. Kissui baada ya mambfunzo kumalizika vizuri

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA