WEMA AMJIBU STEVE NYERERE KUHUSU KURUDI CCM


Staa wa Bongo, Wema Sepetu.
STAA wa Bongo, Wema Sepetu amemfunga mdomo muigizaji mwenzake Steve Nyerere kwa kumwambia hana mawazo ya kurudi CCM kama jinsi ambavyo wengine wanavyofanya.
Wema ameyasema hayo kupitia akaunti yake ya Instagram kujibu ujumbe wa Steve Nyerere aliokuwa ameuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akimkaribisha ndani ya CCM Wakili Alberto Msando ambaye mapema jana alitangaza kujiunga na CCM.
Steve aliandika: “Sasa utakuwa mzalendo wa kweli , Msando naheshimu maamuzi yako maana ni maamuzi sahihi, kwako pamoja na familia yako, rafiki zako nasi tupo pamoja nawe, soon na yuleeeeeeeee rafiki yetu, dada yetu, msanii mwenzetu, naye yupo njiani kurudi nyumbani.”
Hata hivyo Wema Sepetu baada ya kuona ujumbe huo ambao alihisi kama unamlenga, alijibu chini ya ujumbe huo kwa kuandika “I hope hauniongelei mimi… maana mawazo hayo sina.”
Muigizaji Wema Sepetu alihama ndani ya CCM Februari, mwaka huu kwa madai kuwa ameamua kujiunga na Chadema kupigania demokrasia ya kweli.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*