Mfanyabiashara aandaa sherehe ya kuaga kabla ya kufa

Satoru Anzaki at his partyHaki miliki ya pichaNHK
Image captionSatoru Anzaki akiwa kwenye karamu hiyo
Mfanyabiashara mmoja nchini Japan ambaye anaugua saratani na anatarajiwa kufariki karibuni aliwashangaza watu baada ya kuandaa karamu kubwa ya kuaga.
Satoru Anzaki aliwaalika wageni karibu 1,000 wakiwemo marafiki zake, watu waliosoma naye, washirika wake wa kibiashara na wafanyakazi wake.
Satoru, 80, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya kuunda mashine ya Komatsu alipatikana na saratani ya kibofu cha nyongo Oktoba.
"Nimeridhika kwamba niliweza ksuema 'asante' kwa watu niliokutana nao maishani," aliwaambia wanahabari baada ya sherehe hiyo.
"Kwa kuwa nilitaka kufurahia kabisa sehemu ndogo ya maisha niliyobaki nayo, nimeamua nisipokee matibabu baada ya kuzingatia madhara ya tiba," alisema.
Alitangaza mpango wake wa kufanya sherehe hiyo kupitia tangazo gazetini, taarifa ambazo zilisambazwa sana mtandaoni watu wakitaniana kuhusu ingelikuwa wao wangewaalika nani.
Satoru alikodisha chumba katika hoteli moja Tokyo na akaipamba kwa picha za kumbukumbu ya maisha yake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA