MKIKITA KUKITUMIA KITUO CHA YATIMA CHA HOCET KATIKA UTAFITI WA KILIMO HAI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen), Adam Ngamange akiahidi kuchangia sh. milioni moja za kununua vitabu vya maktaba ya shule ya Kituo cha Kulelea Yatima cha Hocet pamoja na kump[eleka mmoja wa yatima katika ziara ya Utalii Kilimo Israel wakati wa harambee ya kuchangia fedha za kununua vitabu vya mkataba hiyo. Harambee hiyo ilifanyika katika Kanisa la KKKT Mtaa wa Milenia, Dar es Salaam.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG-0715-264202


Na Richard Mwaikenda

Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) umeahidi kuanza kukitumia Kituo cha Kulelea Yatima cha Hocet katika mambo ya utafiti wa kilimo hai ili kuingia katika mageuzi ya kilimo chini.

Mpango huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa mtandao huo, Adam Ngamange wakati wa harambee ya kuchangia fedha za kununua vitabu kwa ajili ya Maktaba ya shule ya Sekondari inayoendeshwa na kituo hicho wilayani Mkuranga, Pwani.

"Tunataka kituo hicho kinacholea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi kitumike katika utafiti wa ardhi na mazao kwa kutumia mashine zitakazokuwa zinapima udongo unaofaa kwa kilimo na kupata mavuno mengi yenye ubora unaotakiwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi." Amesema Ngamange.

Amesema kuwa utalaamu huo wameupata walipokuwa kwenye ziara ya utalii wa kilimo nchini Thailand ambapo udongo hupimwa na usiofaa  huwekwa virutubisho ili kuufanya uwe hai utumike hata kwa vizazi vijavyo.

Pia, katika harambee hiyo iliyofunguliwa na Mkuu wa  Jimbo la Magharibu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Mchungaji Jacob Mwangomola, Ngamange alichangia sh. milioni moja ya kununua vitabu kwa ajili ya maktaba na kuahidi kumpeleka mwanafunzi mmoja wa kituo hicho nchini Israel ambako Mkikita imeandaa ziara ya utalii wa kilimo, ili akachote utalaamu wa kilimo unaotumika huko na kuja kuwafundisha wenzie.

Ngamange ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui alipata wasaa wa kuelezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mkikita za kuwaendeleza wakulima na wafugaji kwa kuanzisha mashamba (Block Farm) ya mapapai, muhogo, mchaichai na ufugaji kuku kwa kuwashirikisha wanachama wao wapatao 6000 nchini.Mashamba hayo yanakuwa chini ya uangalizi wa Mkikita kuanzia wakati wa kupanda, mavuno hadi masoko.

Alimazia kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Kituo hicho, Ezekia Mwalugaja ambaye amekiendesha kwa ufanisi kuanzia mwaka 2002 hadi sasa kwa kuwasaidia yatima kielimu ambapo wengine wamemaliza vyuo vikuu na wanajitegemea kimaisha.

Zaidi ya sh. milioni 11 zipatikana katika harambee hiyo, ambapo fedha taslimu zilikuwa zaidi ya sh. milioni 4.5 na ahadi zaidi ya sh. mil. 6.


 Adam Ngamange akionesha kitabu alichokitunga cha Wewe ni Bilonea wa Mtaji Sifuri alipokuwa akiwapiga msasa waalikwa kuhusu masuala ya ujasiriamali wakati wa harambee hiyo. Kutoka kushoto ni Ev na Richard maofisa wa kituo hicho.
 Kwaya ya Kanisa la KKKT Mavurunza ikitumbuiza kwa kwaya wakati wa harambee hiyo.
 Kwaya ya Watoto wa Mungu inayoundwa na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Hocet wakitumbuiza kwa kwaya
 Mkuu wa Jimbo la Magharibi la  KKKT  Dayosisi ya Mashariki na  Pwani, Mchungaji Jacon Mwangomola akihubiri wakati wa ufunguzi wa harambee hiyo
 Kwaya ya Vijana ya Kanisa la KKKT Mavulunza ikitumbuiza
 Mkurugenzi wa Kituo cha Hocet, Ezekia Mwalugaja akitoa neno la shukrani kwa walikwa wote waliofika kwenye harambee hiyo
 Mwalugaja akimpongeza Mrema kutoka Mbeya ambaye alifika kwenye harambee hiyo na kuchangia sh. mil. 2.
 Mmoja wa vijana waliowahi lelewa na Kituo cha Hocet akishukuru na kutoa mchango wake
 Viongozi wa Mkikita, Adam Ngamange na Dk. Kissui wakiwa na baadhi ya waalikwa katika harambee hiyo
 Mrema kutoka Mbeya akijadiliana jambo na Adam Ngamange (kushoto) pamoja na Richard wa Hocet
 Mmoja wa wachungaji waalikwa katika harambee hiyo, akisoma kitabu kilichotungwa na Adam Ngamange kiitwacho Wwewe ni Bilionea  wa Mtaji Sifuri wakati wa harambee hiyo
Adam akiwa na Mkurugenzi wa Hocet, Ezekia Mwalugaja.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

FAHAMU DALILI KUU ZA AWALI ZA MIMBA KUSHIKA

CHANGAMKIA OFA YA KILIMO CHA PILIPILI KICHAA UPATE FAIDA SH. MIL. 50

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.