WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

 Wanahabari na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa
mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Mwananchi, marehemu Joyce Mmasi wakiupeleka kwenye gari baada ya kuwagwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, tayari kusafirishwa kwenda kwa mkoani Kilimanjaro kwa Mazishi. IMEANDALIWA NA RICHARD  MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Joyce Mmasi ukiingizwa kwenye gari tayari kwa safari
kwenda Moshi, Kilimanjaro.
 Marehemu Joyce Mmasi enzi za uhai wake
 Rowlings Nick Maira Mtoto wa kwanza wa marehemu Joyce Mmasi, akisoma wasifu wa mamake
wakati wa kuuaga mwili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Rowlings akiwa na msalaba
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akirtoa salamu za rambirambi wakati wa kuuga mwili wa marehemu Joce Mmasi. Wilaya hiyo iliruhusu viwanja hivyo kutumika kwa shughuli hiyo.
 Rafiki wa karibu wa marehemu Mmasi, mwandishi wa habari mwandamizi, Mashaka Mgeta akielezea sifa alizokuwa nazo marehemu wakati wa uhai wake
 Waombolezaji ambao asilimia kubwa ni wanahabari wakiwa katika shughuli za kumuaga mwenzao, marehemu Mmasi.

 Mashaka Mgeta akiwa na simanzi wakati akitoa sifa alizokuwa nazo wakati wa uhai wa Joyce Mmasi








 Simanzi na Vilio vikiwa vimetawala wakati wa msiba huo




 Baadhi ya wanakamati ya shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu, Mmasi wakitafakari jambo.Kutoka kushoto ni Theophil Makunga, Ibrahim Bakari, Shadrack Sagati, Mgaya Kingoba na Thomson Kasenyenda
 Waombolezaji wakimsaidia mtu aliyezirai wakati wa kuuga mwili wa marehemu
 Waombolezaji wakipita karibu na jeneza wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Joyce Mmasi



 Baadhi ya wanahabari aliowahi fanya nao kazi marehemu Joyce Mmasi katika Kampuni ya Business Times, iliyokuwa inachapisha magazeti ya Majira, Business Times, Majira Jioni, Dar Leo na Sanifu. IMEANDALIWA NA RICHARD  MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG-0715-264202

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA