HATIMAYE KILIO CHA MBUNGE CHATANDA BUNGENI KUHUSU MAJI CHAWAKOMBOA WANAKOROGWE

 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Chatanda (katikati) akiwa na viongozi wa Wilaya ya Korogwe wakikagua maendeleo ya ujenzi wa tanki litakalopokea maji na kuyatawanya mjini.  Pia katika ukaguzi huo walikuwepo viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Geita waliofanya ziara ya kujifunza jinsi miradi mbalimbali inavyotekelezwa wilayani Korogwe

Mradi huo mkubwa wa maji umefanikiwa kujengwa wilayani humo, baada ya Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda kupambana bungeni kwa kuwasilisha kilio cha wananchi kukosa maji ya uhakika licha ya eneo hilo kuwepo na mto mkubwa.

Hatimaye Serikali ilisikia ombi la Mbunge huyo na kutoa fedha za ujenzi wa tanki hilo ambalo hadi ujenzi ulipofikia sasa umegharimu sh. mil. 500, lakini pia bado ujenzi wa miundombinu unaosubiri sh. bil. 2 ambazo serikali iliahidi.

Mradi huo mkubwa unajengwa kwa kutumia mto Pangani  eneo la Mtonga. Tanki hilo litakuwa linapokea maji kutoka kwenye mto huo na kusambaza maji kwa wananchi kwa kutumia miundombinu inayotarajiwa kujengwa.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.