KILWA YAJIPANGA KUBORESHA MIUNDOMBINI YA AFYA


Angela Msimbira- OR TAMISEMI KILWA


Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Dr. Khalfanis Mbukwa amesema kituo cha afya cha Kilwa Msoko ni miongoni mwa vituo 44 vya afya vilivyopatiwa shilingi milioni 500 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) kwa ufadhili wa watu wa CANADA kwa ajili uanzishwaji wa huduma za upasuaji wa dharura kwa akina mama.

Akitoa taarifa kwa Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenye zoezi la ufuatiliaji wa utekelezaji wa ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Dr. Khalfanis Mbukwa amesema majengo yaliyojengwa ni chumba cha kuhifadhia maiti, nyumba ya Mtumishi, maabara, wodi ya akina mama, wodi ya watoto,, jengo la upasuaji na kichomea taka.

Dr.Mbukwa amesema jumla ya shilingi 356,988,598 zilikadiriwa kutumika katika ujenzi huo na mpaka sasa zimetumika shilingi 351,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi, maabara, wodi ya akina mama, wodi ya watoto na jengo la upasuaji.

Amesema ujenzi huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya miundombinu ya afya kwa jamii kwa kuwa awali katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko hakukuwa na Majengo ya Upasuaji, Wodi ya akinamama, wodi ya watoto, maabara na jengo la kuifadhia Maiti kuwa chakavu .

Amesema kuwa Kamati ya Manunuzi, Kamati ya mapokezi ya vifaa na kamati ya ujenzi imejipanga vyema kuendelea kusimamia kwa makini ili kuhakikisha dhamani fedha zilizotolewa na serikali zinaenda sambamba na ujenzi uliokubalika.Aidha ameongeza kuwa kiasi cha fedha kitakachobaki kitatumika kwa ajili ya ujenzi wa uzio,ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), ukarabati wa nyumba za watumishi na ujenzi wa jengo la kiliniki ya Mama, Baba na Mtoto.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi Maiko Makwayi ameipongeza Serikali kuboresha miundombinu ya afya katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko jambo ambalo litasaidia katika kuongeza huduma kwa jamii na kupunguza matatizo ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma.

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Masoko inachangamoto kubwa ya vituo vya afya ameiomba Serikali kuweka kipaombele katika kuboresha vituo vya afya, na Zahanati kwa kuweka miundombinu bora katika Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi ili kupunguza kero hiyo.

Wakati huohuo Katibu wa afya wa Halmashauri ya Wilaya Kilwa Bw.John Maongezi amesema wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa watumishi katika kada ya afya , hivyo ameiomba serikali kupanga watumishi kulingana na ukubwa wa eneo, idadi ya vituo vya afya na idadi ya watu ili kupunguza tatizo hilo kwa Wilaya ya Kilwa.

Aidha Kituo cha Afya cha Halmashauri Kilwa Masoko ni miongoni mwa vituo 5 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya Kilwa na kimezungukwa na zahanati 3 ambazo ni Kisiwani, Mpara Mali ambavyo ni vya Serikali na Zahanati ya Bakwa ambacho ni kituo binafsi na hutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 20,000.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Dr. Khalfanis Mbukwa akitoa taarifa kwa wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya katika Wilaya hiyo.
Moja ya jengo la Wodi ya akinamama lililojengwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Moja ya jengo la upasuaji lililojengwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi
Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Masoko wakimsikiliza Mkuu wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Mathew Mganga(Hayupo pichani) kwenye ufuatiliaji wa Ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya nchini katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA