Korea Kaskazini yafungua mawasiliano ya simu na Korea Kusini


A Korean soldier on the southern side of the border speaks on a telephone, which appears to be heavy-duty and military in natureHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea Kaskazini yafungua mawasiliano ya simu na Korea Kusini
Korea Kaskazini imefungua tena mawasiliano ya simu na Korea Kusini ili kuanzisha mazungumzo kuhusu kushiriki kwake katika mashindano ya msimu wa baridi.
Korea Kusini imethibitisha kuwa ilipata simu kutoka Kaskazini leo Jumatano.
Hii ni baada ya Kim Jong un kusema kuwa ataanzisha mazungumzo na Korea Kusini kuhusu kutumwa timu kwa mashindano ya msimu wa baridi huko Korea Kusini.
Mataifa hayo mawili hayajafanya mazungumzo ya juu tangu Disemba mwaka 2015
The North-South Korea hotline in the village of PanmunjomHaki miliki ya pichaEPA
Image captionKorea Kaskazini yafungua mawasiliano ya simu na Korea Kusini
Mwaka uliofuatia Korea Kaskazini ilikata mawasiliano na kuacha kupokea simu kwa mujibu wa maafisa kutoka Kusini
Afisa kutoka Korea Kaskazini alitangaza kufunguliwa laini hiyo ya simu kwenye ujumbe uliopeperushwa mapema Jumatano.
Mkuu wa idara ya mawasiliano ya raia wa Korea Kusini Moon Jae-in, alisema kuwa kufunguliwa kwa laoni hiyo ya simu kuna umuhimu mkubwa
"Inabuni mazingira ambapo mawasiliano yatakuwa rahisi kila mara," alisema.

Mada zinazohusiana

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA