RAIS MAGUFULI AMEANZA KUAGIZA MABEHEWA YA TRENI YA MWENDO KASI

Serikali kupitia Kampuni Hodhi ya Reli (RAHCO) imetangaza mchakato wa awali wa zabuni ya ununuzi wa vichwa na mabehewa kwa ajili ya treni ya umeme itakayotumika katika reli ya kisasa (Standard Gauge) ambayo ujenzi wake unaendelea.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Masanja Kadogosa ameithibitishia Idara ya Habari (MAELEZO) kuanza kwa mchakato huo ambao unafuata taratibu za kimataifa za ununuzi kwa njia ya ushindani.
Kwa mujibu wa tangazo la zabuni, jumla ya vichwa 14 vya treni ya umeme kwa ajili ya kusafirisha mizigo na vichwa viwili vya treni ya mizigo inayotumia mafuta vinahitajika.
Aidha, RAHCO pia imetoa zabuni ya ununuzi wa vichwa vitano vya treni ya abiria ya kisasa inayotumia umeme (Electric Multiple Units) ambapo kila kimoja kitakuwa na uwezo wa kuvuta mabehewa 60 yenye kuchukua abiria 1,800.
Katika mabehewa hayo ya abiria, mabehewa 15 yatakuwa ni ya kiwango cha daraja la kwanza na mengine 45 ni daraja la pili.
Mbali na mabehewa ya abiria, zabuni hiyo inajumuisha ununuzi wa mabehewa mengine zaidi ya 1,500 yenye muundo tofauti kwa ajili ya kubebea aina mbalimbali za mizigo.
Pamoja na sifa mbalimbali zilizo ainishwa katika tangazo la zabuni, moja ya sifa za reli hiyo ya kisasa ni kuhimili treni ya abiria yenye uwezo wa mwendo kasi wa kilometa 160 na mabaehewa yenye juma ya urefu wa mita 2000, wakati ile ya mizigo yenye uwezo wa kwenda kasi ya kilometa 120 kwa saa.
Kwa mujibu wa tangazo la zabuni, mwisho wa kuwasilisha nyaraka za zabuni ni Januari 30, mwaka huu.Tayari awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hii kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro inaendelea na wakati huo huo tayari Serikali imesaini mkataba kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi kutoka Morogoro hadi Makutupola mkoani Dodoma.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU