TANZIA;MPIGANAJI ATHUMAN HAMISI AMEAGA DUNIA!!!

TANZIA 
Ndugu yetu, Rafiki yetu na Mpigapicha Athumani Hamisi Msengi amefariki dunia Alfajiri ya leo baada ya kuugua ghafla akiwa Nyumbani kwake Sinza na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhiumbili alipofikwa na umauti asubuhi ya leo.

Marehemu amewahi kufanyakazi vyombo mbalimbali vikiwemo The Guardian, Nipashe na Habari Leo;ambapo kwenye Habari alikuwa Mpiga Picha Mkuu wakati lilipoanzishwa mwaka 2006.

Aidha kwenye kampeni za Urais za JK mwaka 2005 marehemu alikuwa ndiye Mpigapicha rasmi wa mgombea huyo.


Akiwa Habari Leo alipata ajali ya gari barabara ya Kilwa, mkoani Pwani alikoenda kwenye kazi za Vodacom,ajali ambayo ilimsababishia kupooza kuanzia kiunoni kushuka chini. Ugonjwa ambao ulimlaza kitandani tangu wakati huo mpaka kifo chake.

Amewahi kutibiwa hospitali mbalimbali zikiwemo na hapa nchini na Afrika Kusini kwa msaada wa Rais Mstaafu JK.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA