TRA YARAHISISHA USAJILI WA WALIPAKODI.



PICHA NAMBA 1
Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni ya  usajili wa walipakodi.
PICHA NAMBA 2
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya  usajili wa walipakodi inayofanyika nchi nzima kwa lengo la kuongeza idadi ya walipakodi, kupanua wigo wa ulipaji kodi na kuongeza mapato ya Serikali.
PICHA NAMBA 3
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (kulia) Bi. Regina Urio akimhudumia mfanyabiashara (kushoto) aliyefika katika kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).
(PICHA ZOTE NA MPIGA PICHA WETU).
………………………………………………………………………………………
Na: Veronica Kazimoto,-Dar es Salaam.
Wafanyabiashara wanaostahili kulipa kodi kwa njia ya makadirio, watalipa robo ya kwanza ndani ya siku tisini (90) kuanzia siku waliyosajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo wa kulipa kodi hiyo kabla mfanyabishara hajaanza kufanya biashara husika.
Hayo yamesema leo na Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) alipotembelea kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni ya  usajili wa walipakodi.
Kamishna Mwandumbya amesema kuwa, hapo awali wafanyabiashara walitakiwa kulipa robo mwaka ya kwanza mara baada ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) suala lililosababisha baadhi ya watu kushindwa kulipa kutokana na msingi mdogo wa biashara zao.
“Niseme tu kwamba, TRA tumeamua kuboresha huduma zetu kwa kuhakikisha kuwa, walipakodi wapya wanalipa makadirio yao ndani ya miezi mitatu tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo mfanyabiashara alitakiwa kulipa kabla ya kuanza biashara yake”, alisema Mwandumbya.
Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Richard Kayombo, amewataka wananchi wanaoishi maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha  na kusema kuwa, zoezi hilo katika kituo hicho litadumu kwa muda wa wiki moja.
“Tukitoka Manispaa ya Ilala tutaelekea Temeke na baadaye tutaendelea kufungua vituo katika maeneo mbalimbali na wakati huo huo ofisi zetu zinaendelea na kazi hii ya usajili kama kawaida” alisema Kayombo.
Mamlaka ya Mapato Tanzania inafanya kampeni ya usajili wa walipakodi nchi nzima kwa  lengo la kuongeza idadi ya walipakodi, kupanua wigo wa ulipaji kodi na kuongeza mapato ya Serikali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA