DK. KISSUI WA MKIKITA AWATAKA WATANZANIA KUOTA NDOTO KUBWA ZA MAFANIKIO


 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkikita, Dk. Kissui S.Kissui (katikati),  akizungumza katika semina ya mafunzo ya kilimo biashara katika Chuo cha Kilimo cha Canre, Dar es Salaam. 

Na Richard Mwaikenda- Canre, Bonyokwa.

WATANZANIA wametakiwa kuota ndoto kubwa badala ya ndogo ili kupata mafanikio makubwa katika maisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), wakati wa mafunzo ya Kilimo Biashara  kwa walimu na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo, Mifugo na Maliasili (Canre), Dar es Salaam.

"Ukitaka kufanikiwa Ota ndoto kubwa  "Bring Big Dream" , acha kuota ndoto ndogo za kitoto zitakazokuchelewesha kupiga hatua za kimaendeleo," alisema Dk. Kissui ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kiuchumi.

Alisema daima amini kwamba ndoto unayoota itakuletea mafanikio chanya na utakuwa nani mbele ya safari.

Pia, Dk. Kissui, aliataka watanzania kuachana na tabia ya kutegemea chanzo kimoja cha mapato, bali wawe na ujuzi mwingi, na kubuni vyanzo vingi vya kuwawezesha kumudu maisha yao ya kila siku.

Alisema moja jambo litakalowatoa kwenye lindi la umasikini ni Kilimo Biashara chenye mtazamo wa kuanza kutafuta masoko ndipo ulime zao kwa kiwango na ubora unaotakiwa na mnunuzi.

Dk. Kissui alisema kuwa Mkikita inaendesha kilimo kwa kufuata utaratibu huo wa kuanza na masoko halafu ndo kinafuata kilimo. Hivi sasa Mtandao huo unaendesha kilimo cha Papai Salama, Muhogo, Mchaichai na Pilipili kichaa mazao ambayo yote yamepata masoko ya ndani na nje ya nchi. 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG-0715 264202,0754 264203


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.