Chama tawala China chaidhinisha "rais wa maisha"


Xi Jinping walking in front of delegates' tables and empty chairsHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023
Chama tawala cha National People's Congress nchini China, kimeidhinisha marekebisho ya kipengele cha katiba, ya kufutilia mbali uongozi wa mihula miwili kwa Rais wa nchi hiyo.
Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023 na kuendelea kuongoza kwa kipindi kisichojulikana.
Wakosoaji wameonya kuhusiana na hatari ya kuondoa muda wa mihula miwili ya uongozi wa Rais, ambayo ililetwa na Deng Xiaoping mwaka 1982.
Xi Jinping claps, looking slightly to the side of the frameHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionHatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023
Chama hicho kinasema kuwa, mabadiliko hayo yataupa nguvu na kuboresha mfumo wa uongozi nchini humo.
Yeyote anayepinga mabadiliko hayo, kwa hofu kuwa itampa nguvu zaidi mtu mmoja, amezimwa nchini humo.
Waandishi habari walinyimwa idhini ya kuingia Bungeni, kushuhudia zoezi hilo la kupiga kura likifanyika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.