MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakolofanyika Mwanza na Simiyu .


MGENI rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza ametangazwa kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

Mama Samia alitajwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama katika mkutano na wanahabari jijini, Dar 
es Salaam, alipokuwa akizungumzia maandalizi ya Tamasha hilo.

Hata hivyo Msama alisema kutokana na majukumu mengi aliyonayo Mama Samia, kwa niaba yake atawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ambaye tayari amethibitisha.

Mbali ya Waziri Nchemba, aliwataja viongozi wengine watakaohudhuria tamasha hilo kuwa ni; Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Angelina  Mabula, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.

Alisema kuwa maandalizi ya Tamasha hilo litakalofanyika Aprili Mosi jijini Mwanza yamekamilika na kwamba wananchi wa Kanda ya Ziwa watarajie kupata uhondo wa muziki wa injili.

Msama amesema kuwa Tamasha hilo la kukata na shoka litatumbuizwa na zaidi ya wasanii mahiri 20 wa hapa nchini na nje ya nchi.Pia katika tamasha hilo albamu mpya ya gwiji wa muziki wa injili Rose Mhando ya 'Usivunjike Moyo.'

Msama, aliwataja wasanii wengine watakaofanya shoo kwenye tamasha hilo kuwa ni, Bonny Mwaitege, Angel Bernard, Christina Shusho, Jesca Honore, Christophre Mhangila, Upendo Nkone na wengine wengi.

Viingilio kwa  wakazi wa Mwanza na maeneo mengine kitakuwa sh. 5000 kwa wakubwa na 2000 kwa watoto na Aprili pili mwaka huu mjini Bariadi, kitakuwa sh. 3000 kwa wakubwa na watoto sh. 2000.

Wakazi wa Kanda ya Ziwa wataendelea kupata uhondo wa tamasha lingine litakalofanyika Jumatatu ya Pasaka mkoani Simiyu katika 
Mji wa Bariadi.  

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKO BLOG;0754264202,0754264203,0689425469


 Msama akitangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa Mgeni Rasmi wa Tamasha la Pasaka atakauwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan atakayewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
 Wanahabari wakiwa kazini
Mratibu wa Tamasha la Pasaka,  akielezea kuhusu maandalizi ikiwemo masuala ya ulinzi na usalama wakati wote wa tamasha.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

DK MAGUFULI AZISAMBARATISHA NGOME ZA MBOWE, NDESAMBURO NA NASSARI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

WAKIANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA, MBOZI