MKIKITA YACHANGIA MIL 2 UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania Mkikita), Adam Ngamange akipewa mkono wa  shukrani na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu pamoja na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya kuahidi kutoa sh. mil. 1 za kusaidia ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza.

Na Richard Mwaikenda, Masaki

MTANDAO wa Kijani Kibichi Tanzania   (Mkikita) umechangia sh. mil. 2 katika harambee ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange aliahidi kutoa sh. mil. 1 kusaidia ujenzi huo, ambapo Meneja Uhusiano wa Mtandao huo, Neema Ngowi aliahidi kutoa sh. mil. 1zitakazochangangwa na wanachama wa

Mkikita.Viongozi hao walitoa ahadi hizo wakati wa harambee iliyofanyika kwenye Hoteli ya
Golden Tulip, Masaki, Dar es Salaam jana, ambapo mgeni rasmi alikuwa  Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan.

Baada ya viongozi hao kuahidi, mshereheshaji wa hafla hiyo, Charles Mwakipesile, aliwaruhusu kwenda meza kuu kupeana mkono wa shukrani na Makamu wa Rais, Samia pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella.

Viongozi wengine waliopeana nao mikono ni Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Mbunge wa Jimbo la Muheza, Rajab Adadi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu.

Ngamange pia aliahidi kuandaa semina ya mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi wa wilaya ya Muheza, ambapo wataweka kambi ya wiki moja wilayani humo kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi.

Pia Mtandao huo wakati wa maandalizi ya harambee hiyo, ulisaidia kumuandalia  Mkuu
wa Wilaya, Mhandisi Tumbo mahojiano maalumu kwenye vituo mbalimbali vya Televisheni ambavyo ni Clouds TV, Azam TV pamoja na mkutano na vyombo vya habari ambapo alizungumzia maandalizi ya harambee hiyo. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0689425467,0754264203 Meneja Uhusiano wa Mkikita, Neema Ngowi akitka kupeana mkono wa shukrani na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada kuahidi kutoa mchango wa sh. mil. 1 zitakazochangangwa na wanachama wa mtandao huo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo,
 Ngamange akijadiliana jambo na Neema
 Ngamange akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (kushoto) pamoja na PRA wa Mkikita, Neema.
 PRO wa Mkikita, Neema Ngowi akiahidi kuchangia sh. mil. 1 kuchangia ujenzi huo
 Adam Ngamange, akiahidi kuchangia sh. mil 1

Wakipata msosi pamoja na wageni wengine waalikwa
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

DK MAGUFULI AZISAMBARATISHA NGOME ZA MBOWE, NDESAMBURO NA NASSARI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

WAKIANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA, MBOZI