SERIKALI KUMALIZA MGOGORO WA VIJIJI VINAVYOZUNGUKA KIA



 Waziri OR-TAMSEMI Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Waziri wa Ujenzi Pro.Makame Mbarawe(kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo(kulia) wakijadili jambo wakati wa kikao maalumu cha Utatuzi wa mgogoro wa Vijiji vinavyozunguka Uwanja wa KIA na Kampuni ya KADCO.


 Waziri wa Ujenzi Pro.Makame Mbarawa(Katikati) akizungumza wakati wa Kikao maalumu cha Utatuzi wa mgogoro wa Vijiji vinavyozunguka uwanja wa Ndege KIA na kampuni inayoendesha Uwanja huo KADCO.
 Waziri OR-TAMSEMI Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Waziri wa Ujenzi Pro.Makame Mbarawe(Pili kushoto), Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula(Kwanza kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo(Tatu kulia) wakiangalia ramani za vijiji vinavyozunguka uwanja wa KIA wakati wa kikao maalumu cha Utatuzi wa mgogoro huo.


Waziri OR-TAMSEMI Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Waziri wa Ujenzi Pro.Makame Mbarawe(Pili kushoto), Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula(Kwanza kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo(Tatu kulia) wakiangalia ramani za vijiji vinavyozunguka uwanja wa KIA wakati wa kikao maalumu cha Utatuzi wa mgogoro huo.
..........................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,TAMISEMI  Mhe. Selemani Jafo amekutana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula kujadili mustakabali wa mgogoro wa Ardhi uliopo kati ya wananchi wanaonzunguka eneo la uwanja wa Ndege wa Kia na mwendeshaji wa Uwanja huo Kampuni ya KADCO.

Mgogoro huo unaohusisha zaidi ya kaya 1200 zilizopo katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha zinatakiwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Kaya hizo ambazo zipo katika vijiji vilivyopimwa Kisheria lakini maeneo ya vijiji hivyo yanaingiliana na eneo la uwanja  wa KIA na hivyo kusabisha mgogoro baina ya Menejimentinya Uwanja na wananchi hao.

Hali hiyo ilipelekea kuundwa kwa timu ya Ufuatiliaji na utafutaji wa suluhu ya mgogoro huo ambayo inaundwa na wizara tatu za Tamisemi, Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya ardhi wakuu wa Mikoa miwili ya Kilimanjaro na Arusha pamoja na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali za ardhi na mawasiliano ya anga.

Kupitia kikao hicho kiliziamia kuwa vijiji hivyo vifanyiwe uthamini upya ili wananchi wa maeneo hayo waweze kulipwa Fidia na kuachia maeneo hayo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanja cha ndege.

Kwa Pamoja viongozi hao wamekubaliana kuanza mchakato wa kufuta hati za vijiji hivyo na kuanza mchakato wa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa eneo hilo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mgogoro kati ya wananchi wanaozunguka uwanja wa ndege wa KIA na kampuni ya KADCO umekuwako toka mwaka 1998 na umesababisha misuguano na hisia kali kwa muda mrefu hali iliyosababisha Serikali kuamua kutafuta  ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA