Wasichana 100 waliotekwa na wanamgambo 'waachiliwa huru Nigeria'


Mwanamume atekwa na hisia baada ya kupokelewa kwa baadhi ya wasichana waliotekwa 19 Februari eneo la DapchiHaki miliki ya pichaISAAC LINUS ABRAK
Image captionMwanamume atekwa na hisia baada ya kupokelewa kwa baadhi ya wasichana waliotekwa 19 Februari eneo la Dapchi
Serikali ya Nigeria imesema wengi wa watoto 110 waliotekwa na wapiganaji wa Kiislami kutoka mji wa Dapchi mwezi uliopita wamerejeshwa.
Wizara ya habari nchini Nigeria imesema wanafunzi 101 kati ya 110 walirudishwa mapema hii leo baada ya 'juhudi za kichinichini za hapo awali.''
Jeshi ''lilisimamisha kwa muda'' operesheni katika eneo hilo ili kuhakikisha ''maisha ya watoto hao hayamo hatarini,'' taarifa hiyo imeendelea kusema.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikuzingatia idadi ya wasichana waliofariki na imesema hakuna kikombozi kilicholipwa kwa wapiganaji hao.
Taarifa hata hivyo zinadokeza kwamba wasichana takriban watano walifariki wakiwa mateka, na msichana mmoja ambaye ni Mkristo bado hajasalimishwa na anaendelea kushikiliwa mateka.
Babake msichana huyo amesema anaendelea kuzuiliwa na wanamgambo hao kwa sababu amekataa kuslimu. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, amesema ana furaha kwamba msichana huyo hakuikana dini yake.
Waziri wa habari na tamaduni, Alhaji Lai Mohammed, amesema kwenye taarifa kwamba wasichana hao waliachiliwa ''katika hali isiyo ya kawaida'' na kwa "usaidizi wa marafiki wa nchi hii.''
"Serikali ilikuwa na uhakika kwamba vita na majibizano havingekuwa suluhu kwani ingehatarisha zaidi maisha ya wasichana hao, na mfumo wa kutotumia nguvu ndio uliokuwa umependekezwa," Bw Mohammed aliongeza.
Pia alidokeza kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu wasichana hao hawakukabidhiwa kwa mtu binafsi , ili kutoa idadi rasmi ya wasichana hao.
Wasichana hao walichukuliwa katika shule hii ya mabweni Dapchi, jimbo la Yobe mwezi FebruariHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWasichana hao walichukuliwa katika shule hii ya mabweni Dapchi, jimbo la Yobe mwezi Februari
Mzazi Kundili Bukar aliambia BBC waasi hao wanaoaminika kuwa wa Boko Haram - waliingia katika mji huo kwa masafara wa magari mapema siku ya Jumatatu na kuwasalimisha wasichana hao kwa jamii.
Ramani ya Nigeria
Image captionRamani ya Nigeria
Waasi hao wanaaminika kuondoka mara moja.
Alisema wasichana hao walionekana kudhoofika na kuchoka - licha ya kwamba ripoti zinasema wasichana hao walipata nguvu ya kukimbia na kurudi nyumbani baada ya kuachiliwa huru.
Mzazi mwengine, Manuga Lawal, amesema aliweza kuzungumza na mwanawe ambaye alikuwa miongoni mwa waliotekwa kwa njia ya simu.
Mmoja wa wasichana walioachiliwa, akizungumza kwa simu na mmoja wa jamaa zake, amesema wasichana watano walikangagwa na kufariki walipokuwa wanalazimishwa kuingia kwenye magari na kuondoshwa wakati wa kutekwa.
Msichana huyo amesema walipelekwa msituni hadi kwenye eneo lililokuwa limezungushwa ua. Alipoulizwa iwapo walikuwa wanalishwa vyema, amesema walilazimika kujipikia chakula chao.
Serikali haijazungumzia vifo hivyo.

'Janga la kitaifa'

Wasichana hao walitekwa walipokuwa shuleni siku ya Jumatatu jioni, tarehe 19 , na kundi la waasi ambao walikuwa wameuvamia mji wa Dapchi.
Hapo awali, ilidaiwa kwamba wasichana wengi walikuwa wametoroka na hakuna aliyekuwa ametekwa.
Lakini wiki moja baadaye, viongozi walikiri walikuwa wametekwa na waasi wa Kiislamu.
Wasichana hao wamerejea mapema asubuhiHaki miliki ya pichaISAAC LINUS ABRAK
Image captionWasichana hao wamerejea mapema asubuhi
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alikitaja kisa hicho cha utekaji kama ''janga la kitaifa'' na kuomba radhi familia za wasichana hao, na kudokeza mwezi Machi tarehe 12 serikali ilikuwa ikifanya majadiliano na waasi ili kuwasaidia wasichana hao kuachiliwa huru wala hawakutaka suluhu ya kijeshi.
''Tunajaribu kuwa makini. Ni heri kuwapata wasichana wetu wakiwa hai,'' alisema kwenye taarifa iliyoonekana na shirika la habari la AFP.
Utekaji nyara umezua wasiwasi mara dufu tangu kutekwa kwa wasichana wa Chibok, waliotekwa shuleni katika jimbo jirani mwezi Aprili mwaka 2014.
Jeshi na serikali hapo awali lilikuwa limekana utekaji nyara kwa wasichana wa Chibok, uliotokea kilomita 275 (Maili 170) kusini mashariki mwa Dapchi.
Rais wa zamani Goodluck Jonathan alilaumiwa kwa kutofanya bidii kuwaokoa wasichana wa Chibok.
Utekaji nyara huo ulizua mjadala ulimwengu mzima na kusababisha kampeini kwenye mitandao ya kijamii.
Zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 walitekwa nyara wamesalia ufungwani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.