YANGA KUFANYA MKUTANO MKUU MEI 5 MWAKA HUU



Na Ripota waMafoto Blog, Dar
KLABU ya Yanga inatarajia kufanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka Mei 5 mwaka huu katika ukumbi utakaotajwa hapo baadaye jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ni matokeo ya kikao cha Kamati ya Utendaji cha Yanga kilichofanyika Jumapili ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga, ambacho kimewataka wanachama kujiandaa kwa ajenda zitakazotangazwa baadaye.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa alipozungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani Dar es Salaam.
Mkwasa, amesema kwamba mkutano huo utakuwa maalumu kwa wanachama kujadili masuala mbalimbali na mustakabali wa klabu.
Aidha Mkwasa amesema, wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada za uanachama wao mapema, kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.
“Mkutano utafanyika Mei 5 hapa Jijini Dar es Salaam, wanachama wenye kadi aina zote mbili wataruhusiwa kuingia ukumbuni, kwa maana ya wale wenye kadi za zamani na hizi zinazotolewa sasa kupitia benki ya posta,”amesema Mkwasa, aliyeongozana na Msemaji wa klabu, Dissmas Ten.
Ikumbukwe Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana.
Kabla ya kufikia maamuzi haya, Manji alipitia kwenye misukosuko na Serikali kuanzia Januari hadi Aprili, kwanza akikamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na baadaye akidaiwa kumiliki pasipoti mbili.
Hali hiyo ilisababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kiufadhili Yanga na kufanya wachezaji wakose mishahara kwa kipindi chote hicho kabla ya viongozi wenzake kuanza kufanya jitihada za kulipa taratibu.
Lakini kwa ujumla ni udhamini wa SportPesa ndiyo umekuwa mkombozi wa tatizo la kiuchumi la Yanga baada ya Manji kuondoka, ingawa hali ya kifedha bado si nzuri klabuni na hilo linatarajiwa kuwa miongoni mwa mambo yatakayajadiliwa Mei 5.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.