Atletico Madrid yalazwa, Barcelona yakaribia kushinda la Liga


Atletico Madrid ilicharazwa 3-0 na Real SociedadHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAtletico Madrid ilicharazwa 3-0 na Real Sociedad
Barcelona imesalia na ushindi mmoja pekee kujipatia taji la 25 la ligi ya La Liga baada ya Atletico Madrid kupoteza kwa Real Sociedad.
Kikosi hicho cha Diego Simeone hakikuonyesha mchezo mzuri na kikajipata nyuma wakati Willian Jose alipomaliza pasi iliopigwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United Adnan Januzaj.
Mchezaji wa ziada Juanmi alifunga bao la pili katika saa za lala salama kabla ya kuongeza bao lake la pili katika dakika ya mwisho.
Barcelona sasa itashinda taji la La Liga iwapo itashinda mechi yake dhidi ya Deportivo Lacuruna tarehe 29 Aprili.
Barca ilimaliza ya pili msimu uliopita wakiwa pointi tatu nyuma ya mabingwa watetezi Real Madrid.
Atletico ambao wako pointi 12 nyuma ya Barcelona wanaelekea Arsenal katika awamu ya kwanza ya mechi ya nusu fainali ya kombe la Yuropa tarehe 26 Aprili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU