CEO WA MKIKITA ADAM KUYAFUATA MASOKO YA MATUNDA, MBOGA ULAYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania Adam Ngamange (kulia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Norwe ya Aquacultural, Ari (kushoto) na Giuseppe ambaye ni CEO WA Taasisi ya LoccoZ ya Uswisi alipokutana nao hivi karibuni kwenye Hoteli ya Coral Beach, Masaki Dar es Salaam. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

Na Richard Mwaikenda, Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange anatarajia kupata masoko makubwa ya matunda na mboga mboga katika ziara atakayoifanya mwezi ujao katika baadhi ya nchi za Ulaya.

Ngamange ambaye anatarajia kuondoka nchini Mei 7, mwaka huu, atashiriki kwenye maonesho ya Kilimo Matunda na Mboga mboga katika Mji wa Rimini, Italia yatakayoanza  Mei 8 hadi 11. Katika maonesho hayo anatarajia kukutana na wafanyabiashara wa kubwa wa mazao hayo na baadhi ataingia nao mikataba ya masoko.

Mei 12  hadi13 atakuwa nchini Uturuki  ambako atakutana na viongozi wa Kampuni kubwa ya uzalishaji wa vifaa vya kilimo katika Kanda ya Ulaya iitwayo Anadulo Motor Export.

Pia akiwa nchini Uturuki Ngamange amehakikishiwa na wenyeji wake kukutana na kukutana na wamiliki wakubwa wa maduka ya vyakula (MPA) nchini uturuki, ujerumani na Bosnia. Mei 14 hadi 15 atakwenda nchini Uswisi ambako ataaini mikataba ya ujenzi wa Kijiji Uchumi mkoani Pwani.

"Mkikita inatoa nafasi ya upendeleo kwa wakulima wakubwa 20 kuiingizwa kwenye orodha ya wazalishaji wenye sifa kwa ajili ya mpango wa mikataba ya Masoko Uwekezaji, mipango ambayo tayari MKIKITA umeshawasilisha kwa kampuni ya MPA na sasa tunasubiri taasisi, kampuni au hata mtu binafsi kuingizwa kwenye mpango huo," amesema Ngamange.

"Masoko Uwekezaji ni jawabu kupunguza shida ya teknolojia na mitaji ili kukidhi mahitaji ya soko la maduka makubwa (Super Market), mpango huu umeisaidia sana Brazili kushika hatamu ya kilimo biashara duniani, Tanzania pia inaweza". Amemalizia kusema Ngamange.

Wanaotakiwa kujiunga kwenye mpango huu ni;Mkulima mwenye uwezo wa kulima ekari zaidi ya 100 za Matunda, mboga mboga na viungo katika sehemu moja au kanda moja,hata walio kwenye vikundi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA