Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni 17 Aprili 2018 Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha Diamond Image caption Diamond Platnumz Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video iliyosambaa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kitandani akicheza na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto pia na mwanamke mwingine ambaye hajajulikana,picha zinazoelezwa kuwa hazina maadili. Waziri wa habari,sanaa na michezo Dokta Harrison Mwakyembe amewaambia wabunge ni matokeo ya sheria mpya za mitandao zilizopitishwa mapema mwezi uliopita. Serikali ya Tanzania yamuonya Diamond Awali serikali ilitaja changamoto kubwa inayolikabili taifa ni athari ya utamaduni wa nje katika maadili, mila na desturi za Mtanzania kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu duniani. Ruka ujumbe wa Instagram wa angelasamwel Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa angelasamwel ''Kuna baadhi ya wasanii wetu ambao wamekuwa wakifanya uhuni uhuni ndani ya mitandao jana tumeweza kumkamata mwanamuziki nyota Diamond tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha na vile vile Nandi naye imebidi apelekwe Polisi kuhojiwa tunaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani. "Nitoe wito kwa vijana mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu, hii nchi ina utamaduni wake tunahitaji kuulinda''. amesema Mwakyembe Nandi pia ni mwanamuziki nyota, ambaye picha yake ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa na mwanamuziki wa kiume billnas ambaye inadaiwa kuwa mpenzi wake akiwa kwenye nguo yake ya ndani sambamba na mwenza wake kitandani. Sheria hizi mpya za mitandaoni zimetungwa kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya mitandao hiyo, huku wakosoaji wakisema kuwa sheria hizi zipo kwa ajili ya kukandamiza uhuru wa kujieleza nchini Tanzania. Chemsha bongo: Diamond aliandika nini Twitter akilalamikia kufungiwa nyimbo?

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video iliyosambaa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kitandani akicheza na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto pia na mwanamke mwingine ambaye hajajulikana,picha zinazoelezwa kuwa hazina maadili.
Waziri wa habari,sanaa na michezo Dokta Harrison Mwakyembe amewaambia wabunge ni matokeo ya sheria mpya za mitandao zilizopitishwa mapema mwezi uliopita.
Awali serikali ilitaja changamoto kubwa inayolikabili taifa ni athari ya utamaduni wa nje katika maadili, mila na desturi za Mtanzania kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu duniani.
''Kuna baadhi ya wasanii wetu ambao wamekuwa wakifanya uhuni uhuni ndani ya mitandao jana tumeweza kumkamata mwanamuziki nyota Diamond tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha na vile vile Nandi naye imebidi apelekwe Polisi kuhojiwa tunaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.
"Nitoe wito kwa vijana mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu, hii nchi ina utamaduni wake tunahitaji kuulinda''. amesema Mwakyembe
Nandi pia ni mwanamuziki nyota, ambaye picha yake ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa na mwanamuziki wa kiume billnas ambaye inadaiwa kuwa mpenzi wake akiwa kwenye nguo yake ya ndani sambamba na mwenza wake kitandani.
Sheria hizi mpya za mitandaoni zimetungwa kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya mitandao hiyo, huku wakosoaji wakisema kuwa sheria hizi zipo kwa ajili ya kukandamiza uhuru wa kujieleza nchini Tanzania.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.