Lwandamina Atimka Yanga, Atua Zesco


Kocha wa Yanga, George Lwandamina.
HATIMAYE kocha wa Yanga, George Lwandamina, jana aliwashangaza wengi baada ya kutimka kwenye timu hiyo kimyakimya na kujiunga na timu yake ya zamani Zesco. Lwandamina mwenye miaka 54, alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Zesco na heshima kubwa aliyonayo hapa nchini ni kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, msimu uliopita.

Jana taarifa zilianza kuzagaa kuwa kocha huyo raia wa Zambia ametimka kimyakimya bila kumuaga kiongozi yeyote wa timu hiyo na kuachana na Wanajangwani hao ambao alikuwa anamaliza nao mkataba mwishoni mwa mwezi ujao.
Kikosi cha timu ya Yanga
Chanzo cha ndani kutoka kwenye klabu ya Yanga kinasema kuwa meneja wa timu hiyo alikwenda kumpitia kocha huyu asubuhi ili aweze kwenda naye mazoezini lakini hakumkuta na hakupewa taarifa yoyote kuwa amekwenda wapi.

“Meneja mara zote ndiye amekuwa akimpitia na kwenda naye mazoezini, lakini alipofika asubuhi alikuta kwake kumefungwa na hakuna taarifa yoyote.

“Hii ilishangaza kwa kuwa ni jambo ambalo halijawahi kutokea hata siku moja na ndipo alipofanya mawasiliano na viongozi wengine wa juu,” kilisema chanzo hicho.

Championi lilimtafuta katibu mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa ambaye alisema kuwa anazo taarifa kuwa kocha huyo hayupo, lakini hafahamu alipokwenda kwa kuwa hajamuaga.


“Ninazo taarifa kuwa kocha hayupo, lakini sijui alipokwenda na sisi tunamtafuta,” alisema Mkwasa na kukata simu. Jioni jana, taarifa ilisema kuwa Lwandamina ametua Zambia na kujiunga na kikosi cha Zesco ambapo wana mpango wa kumtambulisha leo.


“Tunafurahi kumtambulisha Lwandamina kama kocha wetu mkuu na ataanza kazi rasmi akichukua nafasi ya Tenant Chembo ambaye alijiuzulu juzi, hatuna shaka kuwa uwezo wake utaisaidia timu hiikuwa bora na kuliteka soka la Afrika,” ilisema taarifa hiyo ya Zesco ambayo imesema pia kuwa kocha msaidizi Noel Mwandila naye ataungana na kocha huyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA