MAANDALIZI AFCON U17 MWAKA 2019 DAR; SERIKALI KUVIKARABATI VIWANYA VYA TAIFA NA UHURU


Na Mwandishi Wetu, DODOMA
SERIKALI imesema itaratibu ukarabati wa miundombinu ya Uwanja wa Taifa na Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya mpira wa miguu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON-U17) ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji mwakani.
Viwanja hivyo viwili vilikarabatiwa hivi karibuni; Uwanja wa Taifa ukukarabatiwa kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya Everton dhidi ya Gor Mahia huku Uhuru ukifanyiwa ukarabati mkubwa wa Sh. bilioni 10 na Kampuni ya Beijing Construction ya China iliyojenga pia Uwanja wa Taifa.
Hayo yameelezwa bungeni mjini hapa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, alipowasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk, Harrison Mwakyembe 

Amesema majukumu mengine yaliyopangwa kutekelezwa mwaka ujao wa fedha ni pamoja na kukamilisha uhuishwaji wa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995, kuendesha kliniki ya wanamichezo iliyoko Uwanja wa Taifa na kuratibu ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo jijini Dodoma.
Amesema wizara hiyo pia itachimba kisima kirefu cha maji safi na kujenga mifumo yake pamoja na kukarabati miundombinu ya kufundishia michezo katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.
“Vilevile, wizara itashirikiana na TFF kuteua viwanja kadhaa vya michezo mikoani na kuvikarabati ili kukidhi viwango vya FIFA ili viwanja hivyo viweze kutumika kwa baadhi ya michezo ya kimataifa kukwepa utani ambao sasa umegeuka kuwa ugonjwa Dar es Salaam na watanzania kutotofautisha kati ya mechi za utani na mechi utaifa," amesema.
Ili kutekeleza majukumu yake kwa mwaka ujao wa fedha, Mwakyembe ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh. bilioni 33.349 kwa ajili ya wizara hiyo.
Kati yake, Sh. bilioni 15.253 ni mishahara, Sh. bilioni 9.396 kwa ajili ya matumizi mengineyo na Sh. bilioni 8.7 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA