MAN CITY YAPIGWA TENA, BARCA NJE UEFA (Pichaz + Video)


Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akiwa hoi.

MANCHESTER City jana waliishindwa tena Liv­erpool baada ya kuambulia kichapo cha mabao 2-1 na kuondolewa kwenye michua­no ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

(Uefa), huku Barcelona akipigwa 3-0 na Roma.
Katika mchezo wa kwanza Man City wali­chapwa mabao 3-0 kwenye Dimba la Anfield wiki moja iliyopita na jana walitakiwa kushin­da mabao 4-0, ili wafu­zu kwa hatua ya nusu fainali lakini wakaishia kupata kipigo hicho.

Hii ina maana kuwa Liverpool sasa wame­fanikiwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza kwa miaka ya hivi ka­ribuni wakiwa wame­wafunga City jumla ya mabao 5-1.

City walianza kwa kushtukiza baada ya kufanikiwa kufunga bao lao pekee kwenye mch­ezo huo katika dakika ya pili tu, kupitia kwa Gabriel Jesus, baada ya mabeki wa Liverpool ku­fanya uzembe.
Hata hivyo, Liverpool walishindwa kuonyesha kiwango chao cha kawa­ida kipindi cha kwanza na kuwaacha City am­bao walitawala mchezo huo na kukosa nafasi kadhaa za wazi.

Katika dakika ya 40, City walifunga bao lakini mwamuzi akalikataa kutokana na kipa wa Liverpool kufanyiwa
madhambi hali iliyomfanya kocha Pep Guardiola kuwafokea waamuzi wakati wa mapumziko na kuondolewa kwenye benchi ambapo kipindi cha pili alikuwa jukwaani.

Kipindi cha pili, City waliingia kama wachovu baada ya kuonyesha kiwango cha chini na katika dakika ya 56, Liver­pool walisawazisha kupitia kwa Moham­ed Salah baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Saidio Mane.

Wakati City wakipambana kutafu­ta mabao mengine, Robeto Firmino alikuwa shujaa baada ya kuifungia timu yake bao la pili katika dakika ya 77 na kuifanya Liverpool kuwa imeshawach­apa City mara tatu msimu huu, baada ya kuwa timu ya pili iliyoifunga kwenye ligi hadi sasa.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Barcelona walishangaza dunia baada ya kuchapwa ma­bao 3-0 na Roma, na kutupwa nje kwa sare ya mabao 4-4, baada ya Barca kushinda 4-1 kwenye mchezo wa kwanza katika Dimba la Camp Nou.

Hii ni mara ya kwan­za Barcelona wanap­ata kichapo kikubwa hivi msimu huu kwenye Ligi ya M a b i n g w a Ulaya na ki­n a k u w a k ama historia kwao.


Edin Dze ­ko alikuwa tena shujaa kwenye timu yake baada ya kui­fungia bao la kwanza katika dakika ya sita tu ya mchezo. Dakika ya 57 staa wa Roma, De Rossi, alii­fungia timu yake bao la pili kwa mkwaju wa penalti.

Wakati Barcelona wakipoteza muda, dakika ya 82 maajabu yalitokea kwenye soka baada ya Manolas kui­fungia Roma bao la tatu kwa kichwa na kuwaamsha mashabiki jukwaani.
Hii ina maana kuwa Roma wamefuzu kwa hatua hiyo kutokana na faida ya bao la ugenini.
ROMA: Alisson 7; Juan Jesus 7, Manolas 7, Fazio 5; Kolarov 5, Nainggolan 6 (El Shaarawy 77, 7) , De Rossi 8, Strootman 7, Florenzi 7; Schick 7 (Under 72, 7), Dzeko 9
Subs not used: Pellegrini, Gonalons, Peres, Skorupski, Gerson
Goals: Dzeko 6, De Rossi (pen) 58, Manolas 82
Booked: Fazio, Jesus
BARCELONA: Ter Stegen 7; Semedo 6 (Dembele 85), Pique 5, Umtiti 5, Alba 6; Busquets 6 (Alcacer 85), Rakitic 6, Sergi Roberto 5, Iniesta 6 (Gomes 81); Messi 6, L Suarez 6
Subs not used: D Suarez, Cillessen, Paulinho, Vermaelen
Booked: Pique, Messi, L Suarez

Manchester City (3-1-4-2): Ederson 6, Walker 6, Otamendi 5.5, Laporte 5, Bernardo 6.5 (Gundogan 74, 6), Fernandinho 7, De Bruyne 7, Silva 6 (Aguero 66, 6), Sterling 7, Jesus 6.5, Sane 7
Subs not used: Bravo, Kompany, Delph, Zinchenko, Foden
Goalscorers: Jesus 2
Booked: Ederson, Bernardo
Manager: Pep Guardiola 4
Liverpool (4-3-3): Karius 6.5, Alexander-Arnold 6.5 (Clyne 81), Lovren 7, van Dijk 6, Robertson 7, Oxlade-Chamberlain 6, Wijnaldum 6, Milner 7, Salah 6.5 (Ings 89), Firmino 8 (Klavan 81), Mane 7
Subs not used: Mignolet, Moreno, Solanke, Woodburn
Goalscorers: Salah 56, Firmino 77
Booked: Mane, Alexander-Arnold, Firmino, van Dijk
Manager: Jurgen Klopp 7
Referee: Antonio Miguel Mateu Lahoz
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

DK MAGUFULI AZISAMBARATISHA NGOME ZA MBOWE, NDESAMBURO NA NASSARI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

WAKIANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA, MBOZI