Mfalme Mswati abadili jina la nchi yake


Swazland new nameHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMfalme Mswati wa eSwatini akiwa na wapambe wake
Malme wa Swaziland kinyume na matarajio ya wengi amebadilisha jina rasmi la taifa lake kutoka kuitwa Swaziland na kuibatiza jina jipya la Ufalme wa eSwatini.
Alitoa tamko hilo wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka hamsini na wakati huo huo taifa hilo likiadhimisha miaka hamsini ya uhuru wake.
Jina hilo jipya, eSwatini, lina maana ya ardhi ya waswaz na limetumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa tatu kwa miaka mingi. eSwati ni jina ambalo mfalme alilitumia alipokuwa akihutubia katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa manmo mwaka 2017 na katika ufunguzi wa bunge la nchini mwake mwaka 2014.
Mfalme Mswati ni miongoni mwa wafalme wa mwisho wa duniani waliobaki k na ametawala tangu tangu mwaka 1986.Wanaharakati wa kutetea usawa wa jinsi wanasema mfumo wa utawala wa nchi hiyo ni wa kushangaza na unawabagua wanawake.
Ramani ya taifa la Swaziland
Image captionRamani ya taifa la Swaziland
Mfalme Mswati wa tatu ametoa sababu kuu ya kubadilishwa kwa jina la nchi yake kuwa kila aendapo katika mikutano ya kimataifa, mataifa mengine wamekuwa wakilichanganya taifa lake na nchi ya Switzerland.
Nao raia wametoa maoni yao juu ya hatua ya mfalme wao na kusema kuwa badala ya kushughulika na jina la nchi yake , badala yake alipaswa kupasua kichwa ni namna gani anaweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo unaodidimia siku hadi siku.
kwa taarifa yako, Mfalme Mswati anajulikana pia kama Ngwenyama kwa lugha ya taifa hilo jina likiwa na maana ya simba , lakini pia anajulikana ullimwenguni kwa tabia yake ya kuoa wake wengi na kwa kuzingatia mavazi ya jadi pamoja na kuthamini mila na desturi.

Mada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI