PUMA YAZINDUA MPANGO WA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI



 Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbande, Dar es Salaam, Nasri Mustafa akumuonesha Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia) picha aliyoichora na kushinda tuzo  ya usalama barabarani 2017, wakati wa uzinduzi wa mpango wa Puma wa  mafunzo ya ya usalama barabarani kwa wanafunzi, jana katika Makao Makuu ya Puma, Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha  Usalama Barabarani Tanzania.Wa pili kushoto ni SajentiHussein Ramadhan Mwalimu wa Trafiki Makao Makao Makuu ya Usalama Barabarani.Imeandaliwa na Richard Mwaikenda.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imezindua kampeni maalumu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa lengo la kueneza elimu hiyo kuanzia ngazi ya chini. 

Kampeni hiyo inayokwenda sambamba na mashindano ya uchoraji michoro ya usalama barabarani imezinduliwa Dar es Salaam jana na ofisa wa Polisi, ASP Mbuya Matibu, kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usala,ma Barabarani.

AKizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, ASP Matibu,  alisema Puma Energy Tanzania, wana mchango mkubwa katika utoaji elimu ya usalama barabarani, hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.

Pia, aliwataka madereva nchini wasiendeshe magari kwa kukariri sheria,  bali wazitambue ili waweze kuzitumia vizuri kupunguza ajali.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema elimu ya usalama kwa wanafunzi ni muhimu, kwani inawapa uelewa wa matumizi ya barabara kwa usalama.

"Tunawaangalia sana watoto wa shule za msingi kwani wao wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani," alisema Corsaletti na kuongeza;

"Hivyo kwa kuwafundisha usalama barabarani tunawapa ufahamu wa kuwajenga katika matumizi salama ya barabara...hiki ndicho kipaumbele chetu."

Alifafanua kwamba baada ya mafunzo  wanafunzi wanapewa nafasi ya kuchora michoro ya usalama barabarani na mshindi pamoja na shule anayotoka wanazawadiwa.

Corsaletti alisema kampuni hiyo ilianzisha mafunzo hayo mwaka 2013 na imeendelea kufanya hivyo hadi sasa kwa kufikia shule 47 na kuwafundisha wanafunzi 60,000 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Geita.

Aliongeza kuwa uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa kiwango cha ajali katika shule zilizopatiwa mafunzo kimepungua.


Corsaletti, alisema kampuni hiyo itaendelea na kampeni ya usalama barabarani na kuahidi kufanyakazi pamoja na Kikosi cha Usalama Barabarani, maofisa kutoka manispaa au wilaya zinakotoka shule  zilizochaguliwa ili kuhakikisha lengo linatimia.



 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia), akimshukuru Mbunja kwa kuzindua mpango huo.
 Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha  Usalama Barabarani Tanzania, akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango huo.



Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange  akiiweka sawa picha iliyochorwa na Mwanafunzi Nasri Mustafa na kushinda tuzo ya Usalama barabarani 2027
 Shemu ya wadau wa usalama barabarani
 Baadhi ya walimu na wanafunzi waliohudhuria uzinduzi huo
 Wanahabari wakiwa kazini
 Sehemu ya wadau wa usalama barabarani
 Mwanafunzi Nasri Mustafa akionesha picha aliyoichora ya usalama barabarani. Picha hiyo ilishinda tuzo ya kwanza 2017

 Wadau wa usalama barabrani wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi a mpango huo
 Mgeni rasmi, Mbunja na Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti wakiwa na furaha
  Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti, Akisalimiana na wadau baada ya uzinduzi
 Wakiwa katika picha ya pamoja


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI