Raia wa Afrika Kusini watoa heshima za mwisho kwa marehemu Winnie Mandela


Raia wa Afrika Kusini wamuaga Winnie Mandela
Image captionRaia wa Afrika Kusini wamuaga Winnie Mandela
Maelfu ya watu wamekusanyika nchini Afrika Kusini kwa mazishi ya mwanaharakati wa kampeni dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo Winnie Madikizela-Mandela.
Maelfu ya waombolezaji walikusanyika katika uwanja wa michezo wa Soweto karibu na mji mkuu wa Johannesburg ambapo Winnie Mandela anazikwa.
Jeneza lake lilifunikwa na bendera ya taifa hilo na rais wa Afrika Kusini alisoma kumbukumbu ya marehemu.
Bi Madikizela Mandela , ambaye ni mke wa zamani wa Nelson Mandela alifariki mapema mwezi huu akiwa na umri wa miaka 81.
Maria Nyerere anavyomkumbuka Winnie Mandela
Bi Madikizila Mandela alipongezwa kwa mchango wake wakati wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi nchini Afriika Kusini.
Lakini baadaye aliipuuzwa na wanasiasa wakuu kwa kuunga mkono mauaji ya majasusi wa serikali.
Winnie Mandela alikuwa nani hasa?
Mwana wa Madikizela Mandela , Zenani Mandela Dlamini aliwashutumu wale aliotaja walikuwa na kampeni mbaya ya kumchafulia jina mamake na kumtenga kabla ya kumsafishia jina baada ya kifo chake.
''Inakera kuona vile walivyomchukulia wakati wa maisha yake, wakijua vile walivyomuumiza. Wanajua ni kwa nini waliamua kuanza kusema ukweli baada ya kifo chake'', alisema Bi Mandela Dlamini.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA