Rais Magufuli awataka Watanzania kutolalamika kuhusu njaa


John Pombe MagufuliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJohn Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa raia wa Tanzania hawafai kulalamikia njaa wakati ambapo kuna mvua ya kutosha mbali na kwamba serikali inawajengea barabara mpya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wa barabara kuu ya Dodoma-Babati katika eneo la Kondoa, Magufuli alisisitiza kuwa Tanzania haifai kutarajia msaada wa chakula wakati ambapo kuna mvua na barabara.
''Musilalamikie njaa ama kusubiri misaada wakati ambapo taifa lina hali nzuri ya hewa huku barabara zikiendelea kujengwa'', alisema tumieni barabara na mvua kujipatia kipato.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, serikali ya Tanzania inatumia shilingi bilioni 107.6 kuhusu barabara kuu mpya ikiwa ni miongoni mwa ufadhili wa barabara wa shilingi bilioni 378.4 kutoka kwa shirika la msaada nchini Japan Jica na benki ya African Development Bank kulingana na rais Magufuli.
Barabara hiyo mpya yenye urefu wa kilomita 10,228 itapitia mataifa manane ikiwemo Afrika Kusini, Zimbabwe, zambia, Tanzania, Kenya, Sudan, Ethiopia hadi Misri.
Nchini Tanzania barabara hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 1,222 na inatarajiwa kuchukua miaka 20.
Mvua kubwa inayonyesha Tanzania hivi sasa imetatiza huduma za usafiri kwa mabasi ya mwendokasi.
Usafiri wa mabasi hayo umesitishwa kutokana na mafuriko eneo la Jangwani.
Muandishi wa BBC Mjini Dar es Salaam anaeleza kuwa kila mvua kubwa inaponyesha huduma za mabasi hayo husitishwa kutokana na sababu kadhaa.
Mojawapo ya sababu ni kufurika maji kwa njia ambazo mabasi hayo yanapitia na pia kufurika maji kwenye kituo hicho kikuu ambapo mara ya mwisho mabasi kadhaa yaliharibika sababu ya kujaa maji.
Sababu nyingine ni kukatika kwa umeme kwenye vituo vyake wakati wa mvua - hivyobasi kusababisha kukwama kwa mfumo wake wa ukataji tiketi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA