Jérôme Hamon apandikizwa uso wa tatu katika upandikizaji mpya
Image captionJérôme Hamon apandikizwa uso wa tatu katika upandikizaji mpya
Mtu wa kwanza duniani kupandikizwa nyuso mbili amesema kuwa anahisi vyema miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
Uso wa kwanza wa Jerome Hamon ulitolewa mwaka uliopita baada ya kupata ishara za kukataliwa kufuatia matibabu ya dawa ya antibiotic wakati aliposhikwa na homa.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alisalia hospitalini mjini Paris bila uso kwa miezi miwili huku mfadhili wake akitafutwa.
Alisema: Uso wake wa kwanza aliukubali mara moja .Bwana Hamone anaugua ugonjwa unaosababisha uvimbe katika uso.
Upandikizaji wake wa kwanza 2010 ulifanikiwa , lakini akaambukizwa homa 2015 na kupewa dawa za antibiotics.
Dawa hiyo haikuingiliana na matibabu yake hatua iliosababisha damu yake kuukataa uso huo.
Ishara za kwanza za uso huo kukataliwa na damu zilianza kufichuka 2016 na Novemba iliopita. Ilibidi uso huo kuondolewa.
Bwana Hamon aliishi bila uso katia chumba kimoja katika hospitali ya Groges-Pompidou mjini Paris bila kuwa na uwezo wa kuona ,kuzungumza ama hata kusikia hadi mwezi Januari wakati ambapo mfadhili wa uso wake alipatikana na upandikizaji wa pili kufanywa.
Ili kuzuia uso huo kukataliwa na damu yake, bwana hamon aliyepewa jina Mtu mwenye 'nyuso tatu' na vyombo vya habari vya Ufaransa alipatiwa matibabu maalum kusaficha damu kabla ya upasuaji huo kufanyika.
Uso wake wa tatu ni mzuri ijapokuwa fuvu lake la kichwa , ngozi na vipengee vyake havijaingiliana vyema. lakini anaamini kwamba atapona.
''Iwapo ningekataa uso huu mpya ingekuwa vibaya sana . Ni Swala la utambulizi, lakini sasa tumefanikiwa ni vyema kwangu'', aliambia chombo cha habari cha AFP kutoka hospitali ambapo anaendelea kujiuguza.
''Mimi nina umri wa miaka 43 na mfadhili wangu ana miaka 22 kwa hivyo nimerudi kuwa na miaka 22'', aliambia runinga ya Ufaransa.
Upuasiji huo uliochukua saa kadhaa uliongozwa na Profesa Laurent Lantieri , mtaalamu wa upandikizaji wa uso na mikono ambaye alimfanyia upasuaji wa kwanza bwana Hamon miaka minane iliopita.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionUpuasiji huo uliochukua saa kadhaa uliongozwa na Profesa Laurent Lantieri , mtaalamu wa upandikizaji wa uso na mikono ambaye alimfanyia upasuaji wa kwanza bwana Hamon miaka minane iliopita.
Upuasiji huo uliochukua saa kadhaa uliongozwa na Profesa Laurent Lantieri , mtaalamu wa upandikizaji wa uso na mikono ambaye alimfanyia upasuaji wa kwanza bwana Hamon miaka minane iliopita.
''Leo tunajua kwamba upandikizaji wa nyuso mbili unawezekana , hauko tena katika taaluma ya utafiti'', aliambia gazeti la Le Parisien
Daktari Bernard Cholley alisema: Mtu yeyote anapopoteza uso wake na baadaye analazimika kusubiri upandikizaji kwa muda usiojulikana hicho ni kitu ambacho hakuna mtu amewahi kufanyiwa.
Nimeshangazwa na ujasiri wa mgonjwa ambaye ameweza kupitia matatizo haya. Upandikizaji wa kwanza wa uso ulifanyika 2005 kaskazini mwa Ufaransa .
Tangu wakati huo, takriban operesheni 40 za upasuaji zimefanyika kote duniani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*