TAMASHA LA PASAKA LAFANA MWANZA


KIRU1
Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba na Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion wakizindua albam ya mwimbaji Rose Muhando inayojulikana kwa jina la “Usife Moyo” kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo waimbaji mbalimbali wa injili wameshiriki katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rose Muhando amefanya mambo makubwa wakati alipotumbuiza moja ya kibao chake kipya cha "Lazima Wakae" kilichomo katika albam yake hiyo ambapo mashabiki walishindwa kukaa jukwaani na kucheza wakati wote alipokuwa akitumbuiza.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika tamasha hilo leo kwenye tamasha hilo ni, Upendo Nkone, Christina Shusho, Beatrice Mwaipaja, Martha Baraka, Joshua Mlelwa, ,Paul Clement, Sifaeli Mwabuka Dan M kutoka Kenya, Christopher Mwahangila,Bonny Mwaiteje, na wengine wengi.
KIRU
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akionyesha albam ya "Usife Moyo" ya Rose Muhando kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion na Kushoto ni Rose Muhando wakishiriki tukio hilo katika Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
1
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akifurahia albam ya mwimbaji Rose Muhando inayojulikana kwa jina la “Usife Moyo” baada ya kuizindua kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kushoto ni Mwimbaji Rose Muhando.
2
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza katika tamasha hilo mara baada ya kuzindua albam hiyo kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion na kushoto ni mwimbaji Rose Muhando pamoja na maaskofu na wachungaji mbalimbali waliohudhuria kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
3
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akimsikiliza Elibariki Kingu Mbunge wa Singida Magharibi wakati wa tamasha la pasaka kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
4
Dk, Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi na Makazi na mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza akizungumza na kuwakaribisha wageni mbalimbali katika tamasha hilo.
5
Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa Msama Promotion Kanda ya Ziwa akisoma risala katika tamasha hilo.
6
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akimpongeza mwimbaji Bonny Mwaiteje wakati alipokuwa akitumbuiza katika tamasha hilo leo.
7
Hapa Bonny Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani.
8
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akicheza na Mwimbaji Bonny Mwaiteje,
9
Nyomi la Tamasha la Pasaka leo
10 11
Mwimbaji Upendo Nkone akiimba huku akicheza na Mkurugenzi wa Msama Promotion.
12
Mwimbaji Joshua Mlelwa akiimba na Mwimbaji mwenzake Martha Baraka.
13
Joshua Mlelwa akifanya mambo makubwa.
14
Christina Shusho akashusha bonge la Burudani.
15
Martha Baraka akiimba na Mashabiki wake,
16 17
Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Dk. Angelina Mabula akimtunza mwimbaji Christopher Mwahangila,
19
Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Dk. Angelina Mabula akikaribishwa na Alex Msama alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
20
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akilakiwa na Mkurugenzi wa Msama Promotion wakati alipowasili kwenye uwanja CCM Kirumba kama Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka.
21
Mwimbaji Rose Muhando akiimba na Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion mara baada ya kuzindua albam yake Usife Moyo
22
Mwimbaji Rose Muhando akifanya mambo makubwa jukwaani.
23
Bony Mwaiteje naye akashusha burudani nzito
24
Chrstopher Mwahangila akamwaga burudani.
25
Upendo Kone akawachezesha mashabiki wake,
26
Sifaeli Mwabuka akaimba nyimbo zake za kusifu na kuabudu ilikuwa ni burudani kabambe sana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU