Tetesi za soka Ulaya Jumapili 15.04.18


Kylian Mbappe, kushoto
Image captionKylian Mbappe, kushoto
Manchester City itamuwania mchezaji wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 18 Kylian Mbappe iwapo klabu hiyo ya Ligue 1 itapatikana kuvunja sheria za matumizi ya fedha za UEFA.
Mchezaji huyo raia wa Ufaransa alijiunga na PSG kwa mkopo wa msimu mrefu kutoka Monaco mnamo Agosti. (Sunday Mirror)
City pia inataka kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Uhispania Thiago Alcantara, mwenye umri wa miaka 27, aliyefunzwa na Pep Guardiola akiwa Barcelona. (Mail on Sunday)
Na City wanapigiwa upatu katika kumsajili Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 18, aada ya Ajax kumueka thamani ya £50m kwa mlinzi huyo wa Uholanzi. (Sunday Mirror)
Thiago AlcantaraHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionThiago Alcantara
Meneja wa Celtic Brendan Rodgers yupo katika orodha ya watu wanne wanaoonekana kumrithi Antonio Conte katika timu ya Chelsea, ambako aliwasimamia vijana na timu achezaji akiba. (Sunday Express)
Chelsea ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29. Real Madrid pia inamuwania mchezaji huyo. (Daily Star Sunday)
Manchester United intafakari uhamisho wa mlinzi wa Leicester City mwenye umri wa miaka 25 Harry Maguire. (Sunday People)
Huenda United wakashindana na Manchester City kusajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Shakhtar Donetsk raia wa Brazil Fred, mwenye umri wa miaka 25. (Sunday Express)
Meneja wa United Jose Mourinho pia anamuwania mchezaji wa Celtic mwenye umri wa miaka 20 Kieran Tierney. (ESPN)
Liverpool inatarajiwa kumsajili mchezaji wa England wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 17 Bobby Duncan, ambaye ni binamu ya kapteni wa zamani wa timu hiyo ya taifa Steven Gerrard na anayehusika katika magezui katika chuo cha ukufunzi cha Manchester City. (Sun on Sunday)
Steven GerrardHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSteven Gerrard
Gerrard, anayeifunza timu ya Liverpool ya wachzaji wasiozidi miaka 18 anapigiwa upatu kumrithi Mick McCarthy huko Ipswich. (Sun on Sunday)
Everton itawasiliana na ajenti Mino Raiola kuimarisha usajili wa wachezaji msimu huu wa joto. Mageuzi yanayotarajiwa pia yatajumuisha kuondoka kwa meneja Sam Allardyce na mkurugenzi wa soka Steve Walsh. (Sunday Mirror)
Allardyce amesema wakatiwake katika klabu hiyo tayari umekuwa na ufanisi baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Swansea mechi iliyochangia klabu hiyo kusogea katika nafasi ya 9 kwenye Premier League. (Sky Sports)
West Ham inataka kumsajili mshambuliaji wa Nice Alassane Plea, lakini mchezjai huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ufaransa ataigharimu klabu hiyo £25m. (Sun on Sunday)
Juventus inakaribia kukamilisha usajili wa mlinzi raia wa Italia mwenye umri wa miaka 28 Matteo Darmian kutoka Manchester United. (Tuttosport, via Sun on Sunday)
Atletico Madrid inasema hakuna aliyewasilisha ombi kumuulizia Antoine GriezmannHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAtletico Madrid inasema hakuna aliyewasilisha ombi kumuulizia Antoine Griezmann
Winga wa Bordeaux Malcom amesema anatamani sana kujiunga na Paris St-Germain. Raia huyo mwenye umri wa miaka 21 wa Brazil awali alihusishwa na kuingia Tottenham. (Le10Sport)
Liverpool inatarajiwa kumpa kandarasi bora mlinzi raia wa England mwenye umri wa miaka 19 Trent Alexander-Arnold. (Sunday People)
Meneja mkurugenzi wa Atletico Madrid Clemente Villaverde anasema hakuna aliyewasilisha ombi kumuulizia mchezaji kiungo cha mbele Antoine Griezmann. Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wea miaka 27 amehusishwa na timu ya Barcelona na Chelsea. (FourFourTwo)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anasema daima amekuwa akimtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Misri Mohamed Elneny asalie katika klabu hiyo, akieleza kuwa mchezaji huyo anaanza kuonyesha mchezo mzuri. (Independent)
Mkuu wa Stoke Paul Lambert anaamini timu yake ilio katika nafasi ya 19 inaweza kuepuka kushushwa daraja iwapo itaiga maadili ya kimchezo ya mtangulizi wake Billy. (Times)

Mada zinazohusiana

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA