TFF ‘YAIBANANISHA’ YANGA HADI HURUMA, ETI IKITOKA ETHIOPIA IUNGANISHE SAFARI KUIFUATA MBEYA CITY MECHI JUMAPILI


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BODI ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema Yanga SC ikirejea kutoka Ethiopita itaunganisha safari hadi Mbeya kwa ajili ya mchezo wake wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City Aprili 22 Uwanja wa Sokoine.
Yanga ipo mjini Hawassa, Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao utafanyika kesho jioni.
Uwezekano wa Yanga kuondoka Ethiopia ni Alhamisi na watafika usiku, maana yake safari ya Mbeya wanaweza kuianza Ijumaa, siku mbili kabla ya mechi yenyewe.
Dhahiri ratiba hii inawabana mabingwa hao watetezi na hata kama watatumia ndege wanaweza kupoteza siku mbili kwenye safari tu kutoka Hawassa hadi Mbeya.   
Wakati Yanga ikibananishwa namna hiyo, Bodi hiyo imeisogeza mbele kwa siku moja mechi ya mahasimu wao, Simba SC dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa Samora mjini Iringa kutoka Ijumaa hadi Jumamosi.
“Mechi namba 202 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Lipuli na Simba iliyopangwa kufanyika Ijumaa, Aprili 20, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa imesogezwa mbele kwa siku moja. Sasa mechi hiyo itachezwa Jumamosi, Aprili 21, 2018 kwenye uwanja huo huo,” imesema taarifa ya Boniphace Wambura, Mkurugenzi wa Bodi.
Sababu iliyotajwa na Bodi hiyo chini ya Mwenyekiti, Clement Sanga ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Yanga kusogeza mbele mechi ya Simba ni wamiliki wa Uwanja wa Samora kuutumia Aprili 20, 2018 kwa shughuli nyingine za kijamii.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

FAHAMU DALILI KUU ZA AWALI ZA MIMBA KUSHIKA

MAFUNZO YA UONGEZAJI THAMANI VIAZI LISHE YAFANA SUGECO

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!