Ushirikiano wa Kihistoria Baina ya Tanzania na Israel Kuimarishwa


 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akizungumza na waandishi  wa habari mara baada ya kuzindua rasmi Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Ayelet Shaked na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Felix Mosha.



 Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Ayelet Shaked akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF), leo Jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Charles Mwijage (hayupo pichani) alipokuwa akizindua kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaa
 Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Ayelet Shaked alipokutana naye jijini Dar es Salaam leo. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 
 Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akiteta jambo na Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Ayelet Shaked alipokutana naye leo jijini Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kushoto ni Balozi wa Israel anayehudumia Afrika Mashariki, Balozi Noah Gal Gendler.
 Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Ayelet Shaked(kushoto) alipokutana naye kwa ajili ya mazungumzo leo jijini Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kutoka kulia ni Mtetezi Mkuu wa Serikali ya Israel, Dr. Yoav Sapir, Balozi wa Tanzania nchni Israel Mhe. Job Masima.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dkt. Adelardus Kilangi akiteta jambo na Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Ayelet Shaked alipokutana naye leo jijini Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 

Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Ayelet Shaked (waliokaribu na bendera) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF) mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*